PATANISHO: ‘I am busy muache kunilazimisha kuzungumza!’ – Paul

Catherine, 28,aliomba apatanishwe na mumewe bwana Paul, 30, ambaye wameishi pamoja kwa miaka sita.

Wawili hao wana mtoto mmoja ambaye amesaia na Catherine. Anasema kuwa mumewe hamshughulikii mwanao.

Aliyepata alama 428 KCPE afanya kazi ya ‘walking scarecrow’ kwa shamba ya ngano

Kulingana na Catherine,

“Alikuwa mgonjwa na akaamua aende akatibiwe nyumbani kwao, na sasa akiwa kule alinyamaza na hakuwa anawasiliana nami. Ilifika mahali nikamaliza shule lakini sikuwa na karo ya kwenda college na kuna mtu ambaye alikuwa anilipie kisha anikate polepole.

Bwanangu aliposkia niko college alianza kusema kuwa nimepata mume mwingine na tangia Mei hajawahi rudi. Isitoshe alipopata nafuu aliniomba nimtumanie nauli lakini kila mara nikituma hajawahi kuja.”

“Noo I’m busy my friend hata kama unapiga kutoka Radio Jambo. Why would you want to force me?” Alisema bwana Paul pindi tu alipopigiwa simu kabla ya kuskika akinung’unika na marafiki zake.

Mwanahabari aliyekejeli ushindi wa Kipchoge akemewa mtandaoni

Hata hivyo Catherine aliongeza akisema,

Kuna msichana ambaye amekuwa akimchukua na kwenda naye kulala naye lodging na isitoshe alikuwa ananiambia kuwa mie ni mke ambaye sijasoma. Nimekuja nimepata kazi ya kufunza hapa na ninapata fedha, nang’ang’ana nipate fedha ili nilipe karo.

Juhudi zetu za kumfikia Paul kwa mara nyingine tena hazikufua dafu na hapo ikabidi tuwaachie wanajambo waweze kumpa Cate mawaidha.

Abdi Guyo asema maisha yake yamo hatarini, aeleza sababu

 

PATANISHO: “Mke Wangu Hatosheki Kimapenzi Wallahi, Damu Yake moto sana”

Tangia tukio la patanisho ambalo lilimhusisha mwanadada Goretti miaka miwili iliyopita, hatujawahi shuhudia patanisho lingine ambalo mwanadada anakiri kuwa na mpango wa kando na kuomba patanisho na bwanake.

Basi ilikuwa zamu yake Maxmillah 29, ambaye aliomba apatanishwe na bwanake Michael, ambaye walikosana mwaka wa 2013 kisha wakatatua shida zao na kurudiana, lakini ndoa yao bado ilijawa na tatizo chungu nzima kwani wawili hao, hawana amani ndani ya ndoa ya miaka tisa na watoto wawili.

“Kuna wakati alinishikia kisu akitaka kuniua na baada ya hayo shughuli ikawa kunifukuza kwake kisa kuniambia nirudi nyumbani, vita hakuna amani hatuongei kwa nyumba.

Kazi ni kupika lakini ajiwekea mwenyewe maji ajipelekea kwa bafu lakini hatuongei. Nakubali nilimkosea na niliomba msamaha. Alikuja akanipata na mwanaume nyumbani lakini hakupata tukifanya kitendo na hapo ndipo shida ilipoanza. Jamaa huyu alikuwa mpenzi wangu na hapo bwanangu akakasirika sana na kunifukuza na hadi wa leo tukikosana ataja tukio hilo.” Alijieleza Maxmillah.

“Niliingia nyumbani nikapata jamaa kwangu akiwa amejifunga towel yangu na hapo tukapigana na yule jamaa akatoroka, kisha bibi yangu akafunganya virago akaondoka. Uchungu ni kupata mtu red handed nyumbani mwangu uchi wa mnyama, juzi naye nikapata ujumbe kwa simu yake ukisema “Usinipigie simu huyu amewasili” na hapo nikakasirika.” Naye bwana Michael alijieleza akiongeza kuwa “Sitaki kulala nawe kuna magonjwa mengi na nashukuru mungu nilipimwa na niko sawa.”

“Huyu mwanamke hakuwa anatosheka kimapenzi wallahi billahi, damu yake ni moto sana” bwana Michael aliongeza kuni kwenye moto uliozidi kuchoma uhusiano wao huku akikataa katakata kutorudiana na mkewe.

“Nimewacha hizo tabia na sitawahi tena rudia tabia zangu. Isitoshe ana bibi wa pili na sijamkataza kuleta bibi wa pili kwani tutaelewana lakini tuishi na amani, siwezi wachia watoto wangu mke mwenza.” Aliendelea kujiteta Maxmillah.

Pata uhondo kamili katika kanda ifuatayo.