'Naheshimu chaguo lako,'Moses kuria amwambia Martha Karua baada ya kujiunga na Azimio

Muhtasari
  • Katika taarifa kwenye Facebook baada ya Karua kujiunga na Azimio, Kuria alisema anaheshimu uamuzi wake
Mbunge wa Gatunndu Kusini, Moses Kuria
Mbunge wa Gatunndu Kusini, Moses Kuria
Image: MAKTABA

Mbunge wa Gatundu Kusini Moses Kuria ametilia mkazo hatua ya kiongozi wa chama cha Narc Kenya Martha Karua kujiunga na vuguvugu la Azimio la Umoja linaloongozwa na Raila Odinga.

Katika taarifa kwenye Facebook baada ya Karua kujiunga na Azimio, Kuria alisema anaheshimu uamuzi wake.

"Ninaheshimu uamuzi wa dada yangu Martha Karua kujiunga na Azimio kama vile alivyoheshimu uamuzi wangu wa kujiunga na Muungano wa Kenya Kwanza. Hatimaye Kenya ndiyo mshindi na demokrasia itashinda. Naomba timu bora ishinde," Kuria alisema.

Mnamo Jumanne, kiongozi huyo wa CCK alimtaka Karua kuchagua upande wa Kenya Kwanza Alliance na kumteua kiongozi wa UDA William Ruto.

"Chagua upande na uvae Jezi yako. Ninatazamia tikiti iliyo karibu ya Ruto-Karua ili kuokoa nchi hii kutoka kwa utawala wa milele wa nasaba na kutoa matumaini kwa mamilioni ya watoto ambao alienda shule bila viatu," alisema.

Kuria, hata hivyo, alithibitisha kuwa Karua bado atasalia kuwa mshirika wake wa karibu endapo atachagua kambi nyingine.

"Ukiamua vinginevyo utabaki kuwa dada yangu, mkubwa wangu na rafiki yangu."