Raila akita kambi Busia kunadi sera zake

Muhtasari

• Kinara wa ODM Raila Odinga anaelekea katika kaunti ya Busia siku ya Ijumaa huku akitafuta kudhibiti eneo ambalo lilimpigia kura nyingi katika chaguzi zilizopita.

• Siku ya Alhamisi, Raila alimpokea Gavana wa Kajiado Joseph Ole Lenku pamoja na wakilishi wadi 15 waliohama chama cha Jubilee.

Image: TWITTER// RAILA ODINGA

Kinara wa ODM Raila Odinga anaelekea katika kaunti ya Busia siku ya Ijumaa huku akitafuta kudhibiti eneo ambalo lilimpigia kura nyingi katika chaguzi zilizopita.

Katika ziara yake katika kaunti hiyo, Waziri Mkuu huyo wa zamani anatarajiwa kukutana na wakazi wa kaunti ndogo za Teso Kaskazini na Kusini.

Ziara ya Ijumaa ni mwanzo wa kampeni za siku nne za Raila katika eneo la Magharibi mwa Kenya.

Kiongozi huyo wa ODM amekuwa akipokea viongozi kutoka kanda hiyo, na pia kutoka mikoa mingine kote nchini ambao wanajiunga na Vuguvugu la Azimio la Umoja.

Mnamo siku ya Alhamisi, Raila alimpokea Gavana wa Kajiado Joseph Ole Lenku pamoja na Wabunge 15 wa Bunge la Kaunti waliohama chama cha Jubilee.

""Governor of Kajiado County @joelenku ditches Jubilee Party for the ODM. Also defecting are 10 MCAs who accompanied him to Chungwa House. The team was officially received into the party by PL @RailaOdinga,"  chama hicho kilisema.

Kiongozi huyo wa Azimio awali alikutana na viongozi kutoka Kakamega kabla ya ziara yake katika kaunti hiyo.

Walijumuisha; wabunge Oscar Nabulindo, Titus Khamala, Emmanuel Wangwe, Tindi Mwale, Chris Aseka, na Bernard Shinali miongoni mwa wengine.