Robert Alai asalimu amri ubunge wa Nyando kuwania MCA Kileleshwa

Muhtasari

• Robert Alai ametagaza rasmi kwamba atakuwa anawania uwakilishi wadi wa eneo la Kileleshwa.

• Hii ni baada ya mazugumzo na chama cha ODM.

Mwanablogu Robert Alai ametangaza rasmi kwamba atawania kiti cha MCA katika wadi ya Kileleshwa katika uchaguzi wa Agosti 9.

Alai atawania wadhfa huo kupitia tikiti ya chama cha ODM.

Kupitia ujumbe aliochapisha katika ukurasa wake wa Facebook, Alai alisema kwamba uamuzi huo ulijiri baada ya mashauriano na chama cha ODM.

"Kutokana na mazugumzo yanayoendelea katika chama cha ODM, Robert Alai atawania wadhifa wa MCA katika wadi ya Kileleshwa," Alai aliandika.

Alai alikuwa ametangaza kuwania kiti cha ubunge katika eneo la Nyando.

Awali katika azma yake ya kuwa mbunge wa Nyando, Alai alikuwa ametoa manifesto yake kuhusu mambo ambayo angewafayia wakazi wa eneo hilo, ila sasa mambo yanaonekana kubadilika.