Raila akutana na Ngilu, Mutua, Kibwana na Karua kuzima joto katika Azimio la Umoja one Kenya

Muhtasari

• Mkutano huo uliofanyika siku ya Alhamisi ulijiri muda mfupi tu baada ya kiongozi wa Maendeleo Chap Chap gavana Alfred Mutua kutishia kuondoka muungano wa Azimio.

• Mkutano huo ulihudhuriwa na magavana Charity Ngilu (NARC), Alfred Mutua  (Maendeleo Chap Chap),  Martha Karua (Narc-Kenya), Kivutha Kibwana wa Muungano Party miongoni mwa wengine wengi.

Viongozi wa vyama mbali mbali chini ya mwavuli wa Azimio one Kenya
Viongozi wa vyama mbali mbali chini ya mwavuli wa Azimio one Kenya

Kinara wa ODM Raila Odinga ameandaa mkutano wa pamoja na vinara wa vyama tanzu vya muungano wa Azimio La Umoja One Kenya.

Mkutano huo uliofanyika siku ya Alhamisi ulijiri muda mfupi tu baada ya kiongozi wa Maendeleo Chap Chap gavana Alfred Mutua kutishia kuondoka muungano wa Azimio One Kenya kwa kile alitaja kuwa kupuuzwa kwa baadhi ya vyama katika muungano huo.

Mkutano huo ambao madhumuni yake yalikuwa kuzima joto katika muungano wa Azimio ulihudhuriwa na viongozi wa vyama mbali mbali wakiwemo magavana Charity Ngilu wa Kitui (NARC), Dkt. Alfred Mutua wa Machakos (Maendeleo Chap Chap), kinara wa NARC Kenya Martha Karua, Prof. Kivutha Kibwana wa Muungano Party, katibu wa chama cha DAP Kenya Dkt. Eseli Simiyu miongoni mwa wengine wengi.

Kulingana na taarifa ya muungano huo mkutano huo ulijadili maswala yanayohusiana na muungano wa Azimio La Umoja One Kenya kabla ya uchaguzi mkuu wa Agosti 9 baadae mwaka huu. 

 Kwa mujibu wa msemaji wa kamapeni za Raila Odinga, Prof. Makau Mutua, miongoni ma maswala yaliojadiliwa ni pamoja na usawa miongoni mwa wanachama wa vyama tanzu na kuhusishwa kwa wanachama wa vyama tanzu kwenye maamuzi ya muungano huo.  

kinara wa chame cha NARC ambaye pia ni gavana wa Kitui Charity Ngilu amethibitisha makubaliano ya mkao wa Alhamisi na kuahidi kuwa muungano wa  Azimio La Umoja One Kenya bado uko imara.  

Alisema kuwa muungano huo hauangazii vyama binafsi na kwamba agenda yake kuu ni kuleta taifa pamoja kwa manufaa ya wakenya wote.  

Katika tarifa iliyotolewa siku ya Alhamisi hakuna eneo litakalotengewa chama chochote.