Mkurugenzi Mtendaji wa Keroche abadilisha jina kuwa Tabitha Keroche kabla ya uchaguzi

Muhtasari
  • Mwaniaji wa useneta wa Nakuru Tabitha Karanja amebadilisha jina lake
  • Mawakili wake wanasema atatambuliwa kwa jina la kampuni yake - Keroche
Tabitha-Karanja
Tabitha-Karanja
Image: HISANI

Mwaniaji wa useneta wa Nakuru Tabitha Karanja amebadilisha jina lake.

Mawakili wake wanasema atatambuliwa kwa jina la kampuni yake - Keroche.

Notisi ya gazeti la serikali inasema ataitwa Tabitha Karanja Keroche. Utambulisho wake wa sasa ni Tabitha Mukami Mungai.

Tabitha atawania kiti cha Seneta wa Nakuru kwa tikiti ya UDA.

Wakati wa hotuba yake, alisema baada ya mashauriano ya muda mrefu na marafiki na familia, aliamua kujiunga na UDA.

Bi Keroche hatakuwa mwanasiasa wa kwanza au wa mwisho kubadilisha jina lake karibu na uchaguzi kama sehemu ya mkakati.