Ruto apata makao makuu mapya

Muhtasari

• Duru zaarifu kuwa chama hicho kilipata jengo hilo mwezi uliopita.

• Ukarabati kwa sasa unaendelea kwa ofi ya kiongozi wa chama Ruto na afisi ile ya mwenyekiti Johnstone Muthama ambazo zitakuwa za kifahari.

• Ruto amekuwa akifanya kazi na kuratibu shughuli zake za kisiasa katika makazi yake rasmi ya Karen.

DP RUTO
Image: DOUGLAS OKIDDY

Chama kinachoongozwa na Naibu Rais William Ruto cha United Democratic Alliance (UDA) kimepata jengo jipya la orofa tano jijini Nairobi kama makao yake makuu mapya.

Jengo la Edulink liko kwenye Barabara ya Ngong.

Jengo hilo lililo sawa na jengo la Pangani la Jubilee litachukua nafasi ya afisi za kiongozi wa chama, mwenyekiti na katibu mkuu.

Duru zaarifu kuwa chama hicho kilipata jengo hilo mwezi uliopita.

Naibu rais, ambaye ni kiongozi wa chama atakaa orofa ya tatu pamoja na mwenyekiti wa chama Johnstone Muthama.

Ukarabati kwa sasa unaendelea kwa ofi ya kiongozi wa chama Ruto na afisi ile ya mwenyekiti Johnstone Muthama ambazo zitakuwa za kifahari.

Katibu mkuu Veronica Maina atakaa orofa ya nne.

Maafisa wengine wa chama na wafanyikazi watachukua sakafu zilizobaki.

Ruto amekuwa akifanya kazi na kuratibu shughuli zake za kisiasa katika makazi yake rasmi ya Karen.

Kupatikana kwa makao makuu mapya kunajiri wakati ripoti zimeibuka kwamba serikali inapanga kumuondoa naibu rais kutoka kwa makazi ya Karen ili yafanyiwe ukarabati.