MC Jessy hatimaye aweka mambo bayana kilichotokea kati yake na DP Ruto

Muhtasari
  • Alisema alitarajia mkutano huo kueleza jinsi watakavyofanya uteuzi, ili kubaini nani watatunukiwa tikiti
MC Jessy na Naibu Rais William Ruto
Image: MC Jessy/INSTAGRAM

Jasper Muthomi, almaarufu MC Jessy, sasa anasema kuwa hakuwa tayari kujiuzulu kutoka kwa azma ya ubunge wa Imenti Kusini chini ya tikiti ya UDA lakini alilazimika kuheshimu agizo lililotolewa na uongozi wa chama.

Akizungumza katika mahojiano na runinga ya Citizen siku ya Alhamisi, Jessy alisema kuwa wao (DP Ruto na viongozi wengine) walikuwa wamepanga mkutano wa kufanya mazungumzo lakini hakutarajia  ajenda ingekuwa kuhusu yeye kutupilia mbali azma yake ya kisiasa.

Alisimulia kuwa ni katika mkutano huo, ambapo Naibu Rais William Ruto alimshawishi asitishe ombi lake.

Alisema alitarajia mkutano huo kueleza jinsi watakavyofanya uteuzi, ili kubaini nani watatunukiwa tiketi.

“Baada ya mazungumzo sikukubali, sikutaka tufanye hivyo, unajua lazima pia uheshimu viongozi waliopo, tulizungumza na makamu wa rais akanitaka nimwachie ombi langu, baadaye nikamkabili alimwambia kuwa jamii yangu haikutaka niunge mkono mtu mwingine yeyote na kutoa tikiti yangu,” alisema mbunge huyo mtarajiwa.

"Nilikuwa nikizungumza na watu wangu nyumbani, nikawaambia Naibu wa Rais alitaka tufanye mazungumzo lakini sio kukata tiketi yangu. Tulikuwa tunaangalia chaguo la kwanza. ambayo ni mazungumzo kabla ya kwenda kwenye uteuzi."

Aliendelea kusema kuwa baada ya ripoti hiyo kutangazwa, alifanya mkutano wa faragha na DP Ruto ili kuafikiana kwa amani juu ya kuondoka kwake kuwa mgombea huru, ambapo DP Ruto alitoa ridhaa yake.