Joho, Munya kupigania ugombea mwenza wa Raila Odinga

Muhtasari

• Kitendawili  cha kumchagua mgombea mwenza wa Raila Odinga kilichukua mkondo mpya Alhamisi pale Jubilee ilipowasilisha majina ya viongozi mbao wanahisi wana ushawishi na nafasi ya juu kuwahi wadhfa huo.

• ODM, Jubilee na Wiperwana  wanachama wawili kila moja huku vyama vyenye ushawishi mdogo vikiruhusiwa kupendekeza mgombea mmoja.

Viongozi wa Azimio la Umoja- One Kenya Alliance
Viongozi wa Azimio la Umoja- One Kenya Alliance
Image: Fredrick Omondi

Kitendawili  cha kumchagua mgombea mwenza wa Raila Odinga kilichukua mkondo mpya Alhamisi pale Jubilee ilipowasilisha majina ya viongozi mbao wanahisi wana ushawishi na nafasi ya juu kuwahi wadhfa huo.

Chama hicho kilipendekeza kuwa waziri wa kilimo Peter Munya na Gavana wa Mombasa Hassan Joho pia wanafaa kujaribishwa katika nafasi hiyo.

 Kamati ya watu saba iliundwa jana kutathmini wagombeaji wote kufikia wikendi hii na kupendekeza majina mawili kwa Raila na Rais Uhuru Kenyatta kwa uamuzi wa mwisho.

ODM, Jubilee na Wiperwana  wanachama wawili kila moja huku vyama vyenye ushawishi mdogo vikiruhusiwa kupendekeza mgombea mmoja.

Kando na Martha Karua, Kalonzo Musyoka wa Wiper, na mfanyabiashara Peter Kenneth, timu hiyo itachunguza kufaa kwa Joho na Munya pia.

Mfanyabiashara SK Macharia anashinikiza Karua. Kitengo cha juu cha maamuzi cha Azimio, kinachojulikana kama Baraza la Azimio na kinachoongozwa na Rais Uhuru Kenyatta, Alhamisi kiliazimia kuunda jopo la kushauri ni nani atakayechukua nafasi ya Raila.

Uamuzi huo, uliowasilishwa hadharani na baraza hilo lenye wanachama 11, ni pigo kwa Kalonzo na timu yake ya Wiper wanasisitiza kwamba nafasi hiyo ilitengwa kwa ajili yao katika mkataba tofauti uliotiwa saini Ikulu.

Jumanne, naibu mwenyekiti wa Wiper Mutula Kilonzo Jnr na Mbunge wa Makueni Dan Maanzo walishutumu Uhuru na Raila kwa usaliti.

“Tulikubaliana kumuunga mkono Raila kwa msingi kwamba Kalonzo ndiye atakuwa mgombea mwenza. Baadhi ya watu ndani ya ODM wamekuwa wakijaribu kukatisha tamaa hiyo. Hakuna sababu nyingine ambayo tungekubali [kujiunga na Azimio],” Maanzo aliambia Star.

Akihutubia wanahabari baada ya kikao cha baraza hilo jijini Nairobi, Mbunge wa Suna Mashariki Junet Mohamed alitangaza kuundwa kwa jopo la ushauri litakalopendekeza wagombea wenza wanaofaa.

Raila na washirika wake, akiwemo Martha Karua wa Narc Kenya, wanatazamiwa kusafiri hadi Marekani Ijumaa kwa safari ya wiki moja.

Tume ya IEBC imesisitiza kuwa vyama vya kisiasa vinapaswa kutaja wagombea wenza wao kufikia Alhamisi, Aprili 28.

Duru za IEBC ziliambia gazeti la Star kwamba tume hiyo ilifanya kikao Jumatano na kuafiki makataa hayo.

Muda uleule ambao sasa unapingwa na vyama vya siasa ulitumika mwaka wa 2017 na vyama vilifuata. Imeibuka, hata hivyo, ratiba za nyakati zingeweza kutupa mirengo mingi ya kisiasa, ikiwa ni pamoja na Kenya Kwanza, kwenye mkia.

Licha ya kusisitiza hadharani kuwa wako tayari kutaja mgombea mwenza, duru zilisema kuwa timu ya Ruto pia iliwasilisha ombi kwa IEBC kuhusu ratiba