Machozi!Bahati adai ameambiwa ajiondowe kama mgombea ubunge wa Mathare wa Jubilee

Muhtasari
  • Bahati adai ameambiwa ajiuzulu kama mgombea ubunge wa Mathare wa Jubilee
  • Bahati aliongeza kuwa watu wa Mathare wapewe nafasi ya kuwa na kiongozi waliyemtaka siku zote
Kevin Bahati,akihutubia wanahabari siku ya JUmatatu Aprili/25/2022 katika hoteli ya Luke Nairobi
Image: WILFRED NYANGARESI

Mwimbaji Kelvin Bahati ametiririkwa na machozi alipoambiwa ajiuzulu kama Mgombea Ubunge wa Jubilee Mathare.

Bahati alikuwa amepewa tikiti kutoka kwa chama cha jubilee kuwania ubunge wa eneo bunge la Mathare.

Bahati alisema kuwa anawaheshimu Uhuru Kenyatta na Raila Odinga lakini wanapaswa kuwapa vijana nafasi.

Aliongeza kuwa Mathare imekuwa ngome ya ODM lakini kwa kuwa anawania kwa tikiti ya Jubilee anaomba nafasi.

Bahati aliongeza kuwa watu wa Mathare wapewe nafasi ya kuwa na kiongozi waliyemtaka siku zote.

"Ninakuheshimu Rais wangu na ninamheshimu Raila Odinga lakini tafadhali uwape vijana wa nchi hii nafasi. Najua Mathare imekuwa ikimilikiwa kama eneo la ODM lakini kwa hili wakati mmoja, wapeni vijana wa nchi hii nafasi. Wapeni watu wa Mathare kiongozi ambaye wamekuwa wakimtaka siku zote," Bahati alisema.

Mwimbaji Kelvin Bahati aliongeza kuwa watu wa Mathare wamekuwa wakiteseka muda wote na kwa mara moja watu wa Mathare wanahitaji kiongozi ambaye anatoka kwao.

Alimalizia kauli yake kwamba, hakujiunga na siasa ili kupata kazi kwani tayari alikuwa na kazi na ajenda yake ilikuwa kuwasaidia watu wa Mathare.

"Nataka kusema kwa unyenyekevu kwamba Bw.Rais, kiongozi wa chama changu Uhuru Muigai Kenyatta na Raila Odinga, sitawadanganya, watu hawa wa Mathare  niliteseka sana, sikuja kwenye siasa kwa sababu nilitaka Kazi ambayo tayari ninayo, lakini watu hawa wa Mathare wanahitaji kiongozi anayeweza kuwaelewa na matatizo yao. Mtu anayetoka kwao," Bahati alisema.