logo

NOW ON AIR

Listen in Live

DP Ruto ajipigia debe Trans-Nzoia

Ruto anatarajiwa kufanya mikutano katika kaunti ya Trans-Nzoia na Uasin Gishu.

image
na Samuel Maina

Uchaguzi08 May 2022 - 09:54

Muhtasari


  • •DP Ruto anatarajiwa kufanya mkutano wa hadhara kwenye eneo la Matunda Kaunti ya Uasin Gishu.

Mgombea wa wadhifa wa urais kwenye Muungano wa Kenya Kwanza, Daktari William Ruto amewasili katika Kanisa  Katoliki la St. Peter's Clever Kiminini.

Ruto ameandamana na Spika Wa Bunge la Kitaifa Justin Muturi,Kinara wa ANC Musalia Mudavadi, Kiongozi wa Chama cha FORD Kenya, Moses Wetangula, Gavana wa Kaunti ya Trans Nzoia, Patrick Khaemba,  Mbunge wa Bumula, Mwambu Mabonga, Mbunge wa Kiminini, Daktari Chris Wamalwa, Ferdinad Wanyonyi wa Kwanza na Daktari Robert Pukose wa Endebess miongoni mwa viongozi wengine.

Misa inaongozwa na Askofu wa Dayosisi ya Kitale, Anthony Mourice Clowrey.

Baaada ya ibada hiyo Ruto na viongozi wa Muungano wa Kenya Kwanza ataongoza kongomano la kiuchumi kuyakusanya maoni ya wakazi kufanikisha maendeleo ikiwa atachaguliwa kuwa Rais wa tano wa taifa hili.

Mwendo wa saa nane na nusu hivi anatarajiwa kufanya mkutano wa hadhara kwenye eneo la Matunda Kaunti ya Uasin Gishu.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved