Azimio waahirisha ufichuaji wa wagombea wenza walioteuliwa

Muhtasari
  • Azimio yaahirisha ufichuaji wa wagombea wenza walioteuliwa

Jopo la mchujo wa mgombea mwenza wa Azimio limeahirisha kuzindua ripoti yake kuhusu wagombeaji watatu walioteuliwa kuwa mgombea mwenza wa chama hicho hadi Alhamisi.

Kamati hiyo ilitaja kutokuwepo kwa mgombea urais wa Azimio Raila Odinga ambaye yuko Malindi kwa uamuzi wake.

Mwenyekiti wa jopo hilo Noah Wekesa alisema bosi huyo wa ODM atapatikana Alhamisi kupokea ripoti hiyo.

Timu ya uteuzi ilitarajiwa kuwasilisha wagombeaji watatu bora kwa mgombea urais wa Azimio Raila na Rais Uhuru Kenyatta ambao watawachuja watatu hao kwa uamuzi wa mwisho.

Jopo hadi sasa limefanya mahojiano; Kiongozi wa Narc Kenya Martha Karua, kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka, Magavana Charity Ngilu (Kitui), Hassan Joho (Mombasa), Lee Kinyajui (Nakuru) na Wycliffe Oparanya (Kakamega).

Wengine katika kinyang'anyiro hicho ni; Mbunge wa Gatanga Peter Kenneth, Mwakilishi wa Wanawake wa Kaunti ya Muranga Sabina Chege, Balozi wa zamani wa Kenya nchini Australia Stephen Tarus na Waziri wa Kilimo Peter Munya.