Oparanya kuongoza siasa za azimio magharabi

Muhtasari

• Oparanya alikuwa miongoni mwa viongozi 10 waliofika mbele ya jopo la kusaka mgombea wa Azimui siku ya Jumatatu na Jumanne.

• Oparanya alimshukuru Raila kwa kumpa nafasi ya kuongoza na kusema kiongozi huyo wa ODM amejitolea sana kwa ajili ya Kenya, na kumfanya kuwa mgombeaji bora wa urais ili kufufua uchumi wa nchi.

Gavana Wycliffe Oparanya
Gavana Wycliffe Oparanya
Image: THE STAR

Gavana wa kaunti ya Kakamega Wycliffe Oparanya ameteuliwa kuwa mwenyekiti wa kampeni ya Azimio Magharibi.

Oparanya alienda kwenye mitandao yake ya kijamii kutangaza habari hiyo Jumatano.

Aliongeza kuwa tayari ameunda Kamati kwa ajili ya jukumu hilo.

“Tayari nimeunda Kamati ya kampeni ambayo inajumuisha wabunge kutoka maeneo 11 za mkoa ambao nitafanya nao kazi kuratibu kampeni za Azimio,” alisema.

Alisema aliteuliwa wakati wa mkutano wa Nairobi kuweka mikakati ya kuhakikisha kuwa mgombeaji urais wa Azimio Raila Odinga anapata kura nyingi na viti vya uchaguzi kutoka eneo la Magharibi.

Oparanya alimshukuru Raila kwa kumpa nafasi ya kuongoza na kusema kiongozi huyo wa ODM amejitolea sana kwa ajili ya Kenya, na kumfanya kuwa mgombeaji bora wa urais ili kufufua uchumi wa nchi.

Baba (Raila) ndiye mgombeaji bora zaidi wa kukabiliana na ufisadi na changamoto za ukosefu wa ajira na kurejesha utukufu wa nchi iliyopotea,” akasema.

Oparanya alikuwa miongoni mwa viongozi 10 waliofika mbele ya jopo la kusaka mgombea wa Azimui siku ya Jumatatu na Jumanne.

Jumanne, Oparanya alisema ikiwa angepata kazi hiyo, alikuwa akienda kumfanyia kampeni chifu huyo wa ODM ili kuhakikisha atachaguliwa Agosti 9.

"Nikipewa nafasi ya kuwa mgombea mwenza wa Raila Odinga, nitaleta maendeleo yangu na tajriba yangu ya kisiasa kwa timu. Pia nitawaunga mkono kutoka eneo la Magharibi kumuunga mkono Raila kuwa Rais wa tano.