Raila kupokea majina ya waliopendekezwa kwa wadifa wa mgombea mwenza

Muhtasari

Raila ambaye anawania kiti cha urais kwa mara ya tano anakabiliwa na kibarua kigumu kuchagua mgombea mwenza kutoka eneo la Ukambani na lile la Mlima Kenya.

Wadadisi wa siasa wanasema kwamba Raila huenda akalazimika kumtaja mgombea mwenza kutoka kanda ya Mlima Kenya ili kupunguza ushawishi wa Ruto katika kanda ya Mlima Kenya.

Jopo lililoteuliwa kusaka mgombea mwenza wa Raila Odinga katika muungano wa Zamio – One Kenya, leo (Alhamisi) linatarajiwa kumkabidhi Raila majina matatu ya watu waliopendekezwa kwa wadhifa wa mgombea mwanza wa Azimio.

Jopo hilo chini ya uwenyekiti wa aliyekuwa mbunge wa Kwanza Noah Wekesa lilikuwa tayari kumkabidhi Raila majina ya waliopendekezwa lakini Raila alikuwa na shughuli zingine rasmi na kupelekea shuguli hiyo kuahirisha.

Wekesa alisema kwamba Raila aliahidi kuwepo leo ili kupokea mapendekezo ya jopo hilo.

Duru karibu na jopo hilo zilidai kuwa kuna uwezekano mkubwa kwamba watatu waliopendekezwa ni kinara wa Wiper Kalonzo Musyoka, mbunge wa zamani wa Gichugu Martha Karua na aliyekuwa mbunge wa Gatanga Peter Kenneth.

Raila ambaye anawania kiti cha urais kwa mara ya tano anakabiliwa na kibarua kigumu kuchagua mgombea mwenza kutoka eneo la Ukambani na lile la Mlima Kenya.

Wadadisi wa siasa wanasema kwamba Raila huenda akalazimika kumtaja mgombea mwenza kutoka kanda ya Mlima Kenya ili kupunguza ushawishi wa Ruto katika kanda ya Mlima Kenya.

Jopo hilo lilihoji jumla ya wagombeaji tisa kwa wadhifa huo. Waliohojiwa ni Martha Karua, Kalonzo, Magavana Charity Ngilu (Kitui), Hassan Joho (Mombasa), Lee Kinyanji ( Nakuru) na Wycliffe Oparanya ( Kakamega), wengine walikuwa Sabina Chege, aliyekuwa mbunge Stephene Tarus na Waziri wa Kilimo Peter Munya.