Ngirici amtaja aliyekuwa kamishna msaidizi wa KRA Wanjao kama mgombea mwenza

Muhtasari
  • Ngirici alijiondoa katika UDA ya Naibu Rais William Ruto na kuwa mgombea binafsi, akitaja upendeleo

Mwakilishi wa Wanawake wa Kirinyaga, Wangui Ngirici, amemtaja aliyekuwa msaidizi wa kamishna wa KRA Eliud Wanjao Ngige kuwa mgombea mwenza katika kinyang'anyiro cha kiti cha ugavana.

Ngige anatoka eneo bunge la Ndia.

Ngirici alijiondoa katika UDA ya Naibu Rais William Ruto na kuwa mgombea binafsi, akitaja upendeleo.

Mwakilishi huyo wa Kike alidai kuwa licha ya kuwa miongoni mwa wafuasi wa awali wa Ruto, Gavana wa Kirinyaga Anne Waiguru alipendelewa kwa tikiti ya UDA.

Ngirici alizua gumzo alipotoa kauli mbiu yake ya kampeni iliyopewa jina la 'Smairo ni tiki' na alama yake iliyoangazia picha ya meno yake halisi.