Azimio kutangaza mgombea mwenza wa Raila siku ya Jumatatu

Muhtasari
  • Azimio kutangaza mgombea mwenza wa Raila siku ya Jumatatu
Kutoka kushoto Gavana wa Mombasa Hassan Joho, Mbunge wa Suna Mashariki Junet Mohamed na kiongozi wa Narc Kenya Martha Karua katika mkutano wa hadhara 5/5/2022.
Kutoka kushoto Gavana wa Mombasa Hassan Joho, Mbunge wa Suna Mashariki Junet Mohamed na kiongozi wa Narc Kenya Martha Karua katika mkutano wa hadhara 5/5/2022.

Muungano wa Azimio La Umoja-One Kenya kutangaza  mwenza wa Raila Odinga siku ya Jumatatu, Mei 16.

Katika taarifa Jumapili, msemaji wa Sekretarieti ya Kampeni ya Urais ya Odinga Prof.Makau Mutua alisema kuwa uamuzi huo uliosubiriwa kwa muda mrefu hautawekwa wazi Jumapili kama ilivyotarajiwa awali.

"Kampeni yetu inafahamu kuwa Wakenya wana shauku ya kujua tikiti ya urais ya Azimio la Umoja One Kenya. Tutatoa tangazo hilo kesho," aliandika Prof.Mutua.

Wagombea watatu kutoka kwa orodha ya watu 11 waliopendekezwa kwa nafasi hiyo waliwasilishwa kwa mpeperushaji bendera wa muungano huo na jopo la uteuzi, baada ya kufanya mchakato mrefu wa uhakiki.

Majina hayo matatu, jopo lilisema, yalikuwa yamewasilishwa kwa mpangilio wa kipaumbele.

Wagombea waliojitokeza kuchujwa ni pamoja na kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka, Martha Karua (Narc-Kenya), Sabina Chege (Jubilee Party), Peter Kenneth (Jubilee Party) Ali Hassan Joho (ODM) na Stephen Tarus (National Liberal Party).