Wagombea urais waanza kuwasilisha hati za uteuzi kwa IEBC

Muhtasari
  • Wagombea urais waanza kuwasilisha hati za uteuzi kwa IEBC
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) WAFULA CHEBUKATI
Image: EZEKIEL AMING'A

Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka imeanza zoezi la kuwaidhinisha wawaniaji urais katika uchaguzi wa Agosti 9.

Zoezi hilo linafanyika Bomas of Kenya kati ya Mei 29, 2022 na Juni 6, 2022.

Katika ratiba iliyotolewa na Tume hiyo, Peter Kingori na Justus Juma wameratibiwa kuwasilisha karatasi zao za uteuzi kwa IEBC Mei 29, 2022 huku Prof George Wajackoyah na Peter Mongare wakitarajiwa kufika Mei 30, 2022.

Dorothy Kemunto atawasilisha stakabadhi zake Mei 31, 2022. Wengine ni Gibson Nganga (Juni 1), James Kamau (Juni 2), Jeremiah Nyagah, Jane Munyeki na David Mwaure Waihiga (Juni 3).

Mgombea urais wa Kenya Kwanza William Ruto na kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka wameratibiwa kuwasilisha karatasi zao Juni 4, 2022.

Mgombea urais wa Chama cha Muungano Azimio One Kenya Raila Odinga anatarajiwa kuwasilisha stakabadhi zake mnamo Juni 5, 2022.

Dkt Ekuru Aukot na George Munyottah pia wamepangwa kushiriki Juni 5, 2022. Jimi Wanjigi, Muthiora Kiriara na Njeri Kathangu wanatarajiwa Bomas mnamo Juni 6, 2022.

Baada ya kupitishwa, wagombea urais sasa wako huru kufanya kampeni kabla ya uchaguzi.