IEBC imekataa ombi la Prof. Wajackoyah la kutaka kibali cha kuwa mgombea Urais Agosti

Muhtasari
  • IEBC imekataa ombi la Prof. Wajackoyah la kutaka kibali cha kuwa mgombea Urais Agosti
GEORGE WAJACKOYAH
Image: EZEKIEL AMING'A

Mgombea urais wa Chama cha Roots George Wajackoyah amekataliwa na IEBC kwa kukosa kuwasilisha idadi inayohitajika ya saini za wafuasi.

Wakili huyo alikuwa na orodha kamili ya wafuasi kutoka kaunti 17 kati ya 24 zinazohitajika.

Alikuwa miongoni mwa wagombea waliotazamiwa kukutana na Msimamizi wa Kitaifa Wafula Chebukati Jumatatu, katika ukumbi wa Bomas of Kenya.

"Mwenyekiti wa IEBC, Bw Wafula Chebukati amekataa ombi la Prof. Wajackoyah la kutaka kibali cha kuwa mgombea Urais kwa kukosa kuweka sahihi 2,000 zinazohitajika kwa kila kaunti katika angalau kaunti 24. Prof. Wajackoyah ana hadi tarehe 2 Juni saa 3 asubuhi. kukidhi hitaji hilo," IEBC Ilisema JUmatatu.

Wajackoyah ana hadi Alhamisi kuwasilisha sahihi kutoka kwa kaunti saba zilizosalia.