Mbio za farasi 2 kati ya Refigah na mwalimu orero baada ya Refigah kuidhinishwa na IEBC

Muhtasari
  • Katika taarifa, Refigah alisema yuko tayari kutembea pamoja na wananchi ili kubadilisha jamii

Mwanzilishi wa Grandpa records Noah Yusuf, almaarufu Refigah ni miongoni mwa orodha ya wawaniaji walioidhinishwa na IEBC kuwania kiti cha Mbunge wa Kibra.

Refigah anawania chini ya Muungano wa Azimio la Umoja kwenye chama cha DAP-K.

Katika taarifa, Refigah alisema yuko tayari kutembea pamoja na wananchi ili kubadilisha jamii.

"Safari ya kurejesha utukufu uliopotea wa eneo bunge la Kibra imeanza rasmi baada ya kuidhinishwa na IEBC leo nikiandamana na wafuasi wangu wakuu kutoka kila kijiji cha Kibra,"

Kwa kweli ninawashukuru sana wananchi wa kibra kwa kuniamini, kunishika mikono na kunitia moyo katika safari," Alisema

Refigah aliahidi kuhakikisha kunakuwa na maji kwa ajili ya wananchi na kuanzisha taasisi ya mafunzo kwa vijana hao.

"Ni wakati wa kurekebisha. Kibra kupitia uongozi wa watumishi. Uongozi wa watumishi ni kuweka malengo wazi na kisha kukunja mikono na kufanya lolote litakalosaidia watu washinde," alisema.

"Nina rafu nilipanga kila kitu kujitolea maisha yangu kuifanya Kibra kuwa bora zaidi. Mafanikio ni tupu ikiwa unafika kwenye mstari wa kumaliza peke yako. Zawadi bora zaidi ni kufika huko ukiwa umezungukwa na washindi na washindi watakuwa watu wakubwa wa Kibra."

Wengine katika kinyang'anyiro hicho ni pamoja na; Mwalimu Orero wa ODM ambaye pia ameahidi kubadilisha eneo bunge hilo na mshambuliaji wa zamani wa Harambee Stars,Macdonald Mariga.

Pia mwaniaji huyo alisema kwamba Kibra inahitaji kiongozi ambaye anatetea haki za wananchi wa eneo hilo.

Kibra inahitaji kiongozi ambaye anafahamu katiba, kiongozi mwenye sauti ambaye daima atatetea haki zao, kiongozi mwenye mtandao anayeweza kushawishi na kuunda ushirikiano na mashirika yasiyo ya serikali na Coorparate world, kiongozi anayeweza kushiriki katika mazungumzo ya kitaifa kwa masuala yenye maslahi kwa taifa na kiongozi ambaye atatoa elimu ya uraia kwa wapiga kura wake kuelewa bursary kupitia cdf ni haki yao sio upendeleo au chombo cha kampeni na viongozi."

 

Mwanzilishi wa Grandpa records Refigah aidhinishwa kuwania ubunge wa Kibra