Uteuzi wa urais: Wajackoya wafika mbele ya IEBC

Muhtasari

• Kulingana na ratiba ya IEBC naibu rais William Ruto ambaye ni mgombeaji urais kwa tiketi ya chama cha UDA atawasilisha stakabadhi zake za uteuzi Jumamosi 4/6/2022 mwendo saa tano mchana.

Mgombeaji wa urais wa chama cha Roots George Wajakoya akiwasili katika eneo la BOMAS of Kenya kuwasilisha stakabadhi za kuania urais kwa IEBC/EZEKIEL AMING'A
Mgombeaji wa urais wa chama cha Roots George Wajakoya akiwasili katika eneo la BOMAS of Kenya kuwasilisha stakabadhi za kuania urais kwa IEBC/EZEKIEL AMING'A

Baada kipenga kupulizwa kuarishia muda rasmi wa kuanza kwa kampeni za kuania nyadhifa mbali mbali katika uchaguzi mkuu mwaka huu, tume ya uchaguzi na mipaka IEBC inaendelea na zoezi la kupokea stakabadhi za uteuzi za wagombeaji wa nyadhifa mbali mbali.

Shughuli za kupokea stakabadhi za wagombeaji wa urais zilianza siku ya Jumapili 29,5/2022.

Kulingana na ratiba ya IEBC naibu rais William Ruto ambaye ni mgombeaji urais kwa tiketi ya chama cha UDA atawasilisha stakabadhi zake za uteuzi Jumamosi 4/6/2022 mwendo saa tano mchana.

Siku hiyo ya Jumamosi Ruto atafuatwa na kinara wa Wiper Kalonzo Musyoka mwendo wa saa nane alasiri. Hata hivyo bado kuna hali ya ati ati kuhusu uwezekano wa Kalonzo kufika IEBC au ataaamua kurejea katika muungano wa Azimio one Kenya.

Mgombea urais wa chama cha muungano wa Azimio One Kenya Raila Odinga atafika mbele ya IEBC tarehe 5/6/2022 mwendo wa saa nne mchana, akifuatwa na          Ekuru  Aukot wa chama cha Thirdway Alliance.

Mgombeaji wa Roots Party Prof. George Luchiri Wajackoyah anawalisha stakabadhi zake za uteuzi leo Jumatatu.

Wajackoyah ambaye tayari amewasili kwa zoezi hilo alikuwa amevalia bandana kichwani.

Wajackoyah ameahidi kuhalalisha mmea wa bangi ikiwa atachaguliwa kuwa rais.