logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Raila aahidi kuboresha mazingira kwa wawekezaji wa kigeni

Raila Odinga alielezea gharama za juu za nishati nchini Kenya kuwa jambo linawafurusha wawekezaji.

image
na Radio Jambo

Burudani31 May 2022 - 13:46

Muhtasari


• Raila alisema utawala wake mara tu baada ya kuchaguliwa utaomgeza uzalishaji wa nishati kutoka megawati 2,000 za sasa hadi megawati 10,000. 

• Mgombea mwenza wake Martha Karua alikariri kujitolea kwake katika kuhakikisha masuala yote ya kisheria yanayosubiri kushughulikiwa pamoja na sera zinazopendelea wawekezaji.  

Mgombea urais wa muungano wa Azimio One Kenya Raila Odinga akihutubia Baraza la Biashara la Ulaya (EBC Kenya), 31/5/2022.

Kenya inatazamiwa kuangazia sana mambo yanayoathiri sekta ya kibinafsi, miongoni mwao ikiwa ni kodi za juu, kucheleweshwa kwa kesi mahakamani na urasimu, katika jitihada za kuweka mazingira mwafaka kuvutia uwekezaji zaidi. 

Katika mkutano na wajumbe kutoka Baraza la Biashara la Ulaya (EBC Kenya) uliofanyika Westlands Nairobi siku ya Jumanne, Mgombea urais kwa tiketi ya Azimio la umoja Raila Odinga alielezea gharama za juu za uzalishaji wa nishati nchini Kenya kuwa jambo linawafurusha wawekezaji. 

Darren Gillen kutoka Baraza la Biashara la Ulaya (EBC Kenya)

Raila alisema utawala wake mara tu baada ya kuchaguliwa utaomgeza uzalishaji wa nishati kutoka megawati 2,000 za sasa hadi megawati 10,000. 

Raila aliwahakikishia wawekezaji kutoka bara Ulaya kuhusu mipango yake kuanzisha Maeneo Maalum ya utengenezaji wa bidhaa na upanuzi wa miundombinu kimataifa.  

Alisema utawala wake utashughulikia kwa usawa watumishi wa umma wanaomiliki biashara zinazoshindana na sekta binafsi.  

Mgombea mwenza wake Martha Karua alikariri kujitolea kwake katika kuhakikisha masuala yote ya kisheria yanayosubiri kushughulikiwa pamoja na sera zinazopendelea wawekezaji.  

Baraza la Biashara la Ulaya Kenya (EBC Kenya) ndilo shirika mwavuli linaloleta pamoja Mashirika yote ya Biashara, Vyama vya Biashara na Mabalozi wa biashara kutoka mataifa mbalimbali ya Ulaya.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved