Kalonzo apiga U-turn ya mwaka na kurejea kwa Azimio one Kenya

Muhtasari

• Kinara huyo wa Wiper alisema kwamba azma yake sasa ni kuunganisha taifa la Kenya.

• Alisema ataunga mkono kwa dhati uteuzi wa Martha Karua kama mgombea mwenza wa Raila Odinga na atakuwa katika mstari wa mbele kupigia debe muungano wa Azimio.

Kalonzo na Raila Odinga
Image: TWITTER// RAILA ODINGA

Kinara wa Wiper Kaonzo Musyoka amerejea tena katika muungano wa Azimio One Kenya.

Akizungumza baada ya kukutanza na maafisa wa chama cha Wiper siku ya Alhamisi Kalonzo alisema kuwa baada ya kutafakari na kushauriana na wandani wake ameamuka kumuunga mkono kinara wa ODM Raila Odinga.

Kalonzo alisema kwamba amekuwa na muda wa kutosha kutafakari kuhusu hatima yake katika siasa.

“Nimeamua kuahirisha azma yangu kuwa rais wa Kenya kwa manufaa ya taifa,” Kalonzo alisema.

Kalonzo aliongeza kuwa…“Baada ya mashauriano ya kina nimekubali kwa unyenyekevu wadhifa wa waziri mkuu chini ya serikali ya Azimio One Kenya’

Makamu huyo wa rais wa Zamani alisema ataunga mkono kwa dhati uteuzi wa Martha Karua kama mgombea mwenza wa Raila Odinga na atakuwa katika mstari wa mbele kupigia debe muungano wa Azimio.

Kinara huyo wa Wiper alisema kwamba azma yake sasa ni kuunganisha taifa la Kenya.

Makamu huyo wa rais wa zamani alimshukuru mwenyekiti wa Kanu Gideon Moi kwa kusalia naye wakati huu wote alipokuwa akitafakari kuhusu mwelekeo wake mpya kisiasa.