logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mgombea kiti afika mbele ya IEBC akiwa amevalia magunia kuonyesha unyenyekevu

Alisema mtindo wake ni ishara ya unyenyekevu, utumishi na kujitolea kwake kuwahudumia wakazi.

image
na

Habari05 June 2022 - 04:41

Muhtasari


•Tonny Wekesi, 24, aliwashangaza wengi wakati alipoingia katika afisi za IEBC za Eneo Bunge la Saboti ili kupata kibali cha kuwania kiti.

•Alisema mtindo wake ni ishara ya unyenyekevu, utumishi na kujitolea kwake kuwahudumia wakazi wa Matisi ambao wamemfanyia mengi.

Tonny Wekesi

Mgombea kiti cha MCA katika Kaunti ya Trans Nzoia alifika mbele ya IEBC Jumamosi akiwa amevalia magunia ili kuwasilisha stakabadhi zake. 

Tonny Wekesi, 24, aliwashangaza wengi wakati alipoingia katika afisi za IEBC za Eneo Bunge la Saboti zilizo katika Makavazi ya Kitaifa ya Kenya huko Kitale kupata kibali cha kuwania kiti.

Alikuwa akitaka tume ya uchaguzi imuidhinishe kugombea kiti cha MCAMbunge wa Wadi ya Matisi kwenye uchaguzi wa Agosti 9.

"Ninavaa gunia hili ili kuwajulisha wakazi wa Matisi ni aina gani ya uongozi nitawapa nikichaguliwa. Wao ndio chanzo cha msukumo wangu, nitaendelea kuwa na deni kwao milele," alisema.

Nguo za magunia katika Agano la Kale zilivaliwa ili kuonyesha toba na kutafuta kibali cha Mungu wakati wa ukiwa.

Wekesi ambaye ni mtaalam wa IT, alisema kanuni zake za mavazi sio dalili kwamba yeye ni mfuasi wa dhehebu fulani.

Alisema mtindo wake ni ishara ya unyenyekevu, utumishi na kujitolea kwake kuwahudumia wakazii wa Matisi ambao wamemfanyia mengi.

Mgombea kiti huyo mchanga alikuwa miongoni mwa wagombeaji 13 ambao walikuwa wameorodheshwa ili kupitishwa na IEBC Siku ya Jumamosi.

Miongoni mwao ni aliyekuwa MCA Obed Mahanga ambaye alikuwa wa tano kupitishwa na Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo hilo Kennedy Komolkatro.

Wekesi aliwataka wapiga kura kukumpigia kura akiahidi kwamba ataweka utaratibu wa kuwawezesha bila kujali itikadi za vyama vya siasa wanavyojihusisha navo, jamii au kiutamaduni.

Alisema akichaguliwa, atatanguliza uunganisho wa umeme kwenye nyumba, afya na masuala ya elimu.

Mgombea Huru wa wadi ya Saboti Leonard Moss ambaye pia aliidhinishwa alisema atapa kipaumbele utoaji wa hati miliki za ardhi kwa wamiliki wa ardhi.

Moss alisema kipaumbele chake kikuu ni ukombozi wa kiuchumi wa watu wote wanaoishi katika kata ya Saboti bila kujali kabila lao.

Mgombea wa UDA Stephen Matui almaarufu Nyayo pia aliwasilisha karatasi zake za uteuzi katika Makavazi ya Kitale ya Kenya.

Bonface Wanyonyi Cheloti wa Democratic Action Party of Kenya DAP-K pia aliidhinishwa kuwania kiti hicho.

Aliahidi kuanzisha awamu mpya ya uongozi wa kisiasa ambayo itaweka kipaumbele katika uwekaji lami wa barabara ya Kambimiwa–Saboti-Gituamba ili kurahisisha usafiri.

Wengine waliopewa hati safi ya kumrithi David Kipkorir Kapoloman ni Edward Musombi Munabi (Ford Kenya), Wycliffe Masengeli (Independent), Richard Sululu (ANC) na Moses Khaoya (Jubilee).

(Utafsiri: Samuel Maina)


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved