Mgombea urais ateketeza kadi ya wapiga kura baada ya kunyimwa kibali

Muhtasari
  • Mwenyekiti wa tume hiyo Wafula Chebukati alisema mgombeaji huyo aliwasilisha "rundo la nakala za vitambulisho kwa kaunti ambazo hazijabainishwa"
Mwaniaji urais Muthiora Kariara
Image: WILFRED NYANGARESI

Mwaniaji urais Muthiora Kariara ameteketeza kadi yake ya mpiga kura baada ya kunyimwa kibali cha kugombea.

Kariara alijiwasilisha kwa IEBC katika ukumbi wa Bomas of Kenya ili kupata kibali siku ya Jumatatu wakati azma yake ilipogonga mwamba.

Alikuwa mgombea wa mwisho kukataliwa ombi lake baada ya kukosa kufaulu mtihani wa IEBC.

Mwenyekiti wa tume hiyo Wafula Chebukati alisema mgombeaji huyo aliwasilisha "rundo la nakala za vitambulisho kwa kaunti ambazo hazijabainishwa".

Kati ya orodha ya wafuasi 20 ambayo aliwasilisha, Chebukati alisema, ni kaunti 19 pekee ndizo zilizopatikana kutii kanuni zilizowekwa.

Mgombea mwenza wake, aliongeza, hakuwa na kanuni za maadili zilizotiwa saini ambazo ni mojawapo ya stakabadhi za lazima ili kupata kibali. Wengine ni Gibson Ngaruiya, Dorothy Kemunto, James Kamau, Jeremiah Nyaga, Jane Juliet Munyeki, Peter Kingori, na George Munyotta. .

Mgombea wa Ford Asili Njeru Kathangu alikosa kufika mbele ya jopo la mchujo na kusababisha kuondolewa kwake.