logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Kang'ata amteua mgombea mwenza mwingine baada ya hitilafu ya uidhinishaji

Kang'ata aliwashutumu wapinzani wake kwa kuchangia katika dhiki zake.

image
na

Burudani08 June 2022 - 08:18

Muhtasari


•Kang'ata  alifika mbele ya IEBC Jumanne asubuhi ambapo aliwasilisha jina la mgombea mwenza mwingine, Stephen Mburu Munania.

•Timu ya Kang’ata ilianza kutoa mabango yaliyoashiria kuwa mgombea mwenza mpya alikuwa ameteuliwa. 

Seneta wa Murang'a Irungu Kangata

Imeibuka kuwa mgombea ugavana wa Murang’a kwa tikiti ya UDA Irungu Kang’ata alilazimika kuchagua mgombea mwenza mwingine ili aidhinishwe na IEBC. 

Kang’ata alikuwa amepewa hadi Jumanne kuthibitisha kuwa madai yaliyowasilishwa mbele ya IEBC kwamba mgombea mwenza wake Winnie Mwangi hakujiuzulu kwa wakati ni uongo. 

Mgombea huyo alifika mbele ya tume hiyo Jumanne asubuhi ambapo aliwasilisha jina la mgombea mwenza mwingine, Stephen Mburu Munania mwenye umri wa miaka 29.

Alipoulizwa ikiwa madai dhidi ya Mwangi yalikuwa yamefutiliwa mbali, Kang’ata alishindwa kujibu maswali hayo na kwa werevu akaiongoza timu yake kutoka kwenye mahojiano. 

Baadaye aliwashutumu wapinzani wake kwa kuchangia katika dhiki zake. Alisema wapinzani wake waliiandikia IEBC kulalamika kuhusu kujiuzulu kwa Mwangi kwa nia ya kuzuia kibali chake. 

Kwa upande wake, Mwangi alisema timu yao inafuata na isingejihusisha na jambo lolote ambalo ni uvunjaji wa sheria. 

Wakili wa Kang’ata Gachii Mwanza pia alikosa kueleza ikiwa mteja wake alikuwa amemchagua mgombea mwenza baada ya hitilafu ya kibali. 

Lakini baadaye jioni hiyo, timu ya Kang’ata ilianza kutoa mabango yaliyoashiria kuwa mgombea mwenza mpya alikuwa ameteuliwa. 

Kang’ata ambaye ni seneta wa sasa wa Murang’a pia alitoa taarifa kwenye mtandao wake wa kijamii, akimtambulisha mgombea mwenza wake mpya. 

"IEBC ilishiriki malalamishi yaliyotayarishwa na wakili akidai kuwa naibu gavana wetu alishindwa kujiuzulu kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi kwa wakati ufaao." 

“Madai hayo hayakuwa sahihi na yametokana na kutoelewa sheria ya uajiri. Maoni yetu yalikuwa kwamba kujiuzulu kunaanza kutekelezwa kuanzia tarehe ya kuwasilisha barua ya kujiuzulu. Kwa wanaotaka mishahara, inaanza kutekelezwa kuanzia tarehe ya kusitishwa kwa mishahara,” ilisema taarifa hiyo. 

Alisema timu yake ilizingatia kwamba suala hilo lingeweza kuwa mtego wa kesi za muda mrefu ambazo zingeweza kuzivuruga kampeni zake na kukubaliana kwa pamoja kutafuta mgombea mwenza mwingine. 

Mburu anatoka kijiji cha Karega huko Mbugiti, kaunti ndogo ya Gatanga.

 Ana shahada ya Diplomasia ya Kimataifa na amefanya kazi kama Kamishna Msaidizi wa Kaunti, nafasi ambayo aliyoiacha ili kugombea MCA wa Kariara.

 “Winnie Mwangi anasalia kuwa s sehemu ya timu. Ataendelea kutoa huduma zake kama mtaalamu katika masuala ya ardhi,” Kang’ata alisema. 

Wagombea wengine, Wairagu Wa Maai (DP), Joseph Mbai (Usawa Kwa Wote), Henry Gaate (Huru) na Moses Mwangi (Safina Party) walichagua wagombea wenza wa kiume.

(Utafsiri: Samuel Maina)


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved