Ningempigia Wajackoyah kura kama Raila hangekuwa anawania urais-Mutahi Ngunyi

Muhtasari
  • Wajackoyah amekosolewa kwa sababu ya ajenda yake kuhusu bangi, ambayo alisema kuwa ikiwa atashinda uchaguzi wa urais wa Agosti 9 atahalalisha bangi nchini Kenya

Profesa Mutahi Ngunyi amedokeza kupitia ukurasa wake rasmi wa twitter akidai kuwa angempigia kura Wajackoyah katika uchaguzi wa urais wa Agosti 9 ikiwa si kwamba Raila Odinga atawania kiti sawa. .

Kulingana naye Wajackoyah ni mwanamfalme wa kweli ambaye anastahili kura za Wakenya katika uchaguzi wa urais wa Agosti 9.

"Kama Baba hangegombea, ningempigia kura Wajackoyah kuwa rais wa 5 wa Kenya ili tu nipoteze kura yangu. Mtu huyu ametoa sauti kwa Roho ya Giza ya Wakenya. Hakika ni sio kupoteza mawazo ya Taifa letu," Profesa Mutahi Ngunyi aliandika.

Wajackoyah amekosolewa kwa sababu ya ajenda yake kuhusu bangi, ambayo alisema kuwa ikiwa atashinda uchaguzi wa urais wa Agosti 9 atahalalisha bangi nchini Kenya.

Wajackoyah ambaye alivuma sana kutokana na ahadi yake ya kuhalalisha bangi, alisema ufugaji wa nyoka ni mradi wa faida ambao serikali yake itazingatia iwapo atachaguliwa katika uchaguzi wa Agosti 9.

Alifichua kuwa sumu ya nyoka ambayo inaweza kutolewa kutoka kwa nyoka wanaofugwa ina thamani kubwa ambayo inaweza kuendesha uchumi wa nchi sambamba na kilimo cha bangi.

"Tunaanzisha ufugaji wa nyoka nchini ili tuweze kukamua sumu ya nyoka kwa madhumuni ya dawa, watu wengi wanaumwa na nyoka hapa nchini na inabidi msubiri dozi kutoka nje ya nchi kupitia shirikisho la dawa," Wajackoya alisema katika mahojiano na Citizen TV Jumatano jioni.

Wajackoyah alisema baada ya utoaji wa sumu nyoka hao watasafirishwa nje ya nchi kama chakula kwa nchi zinazokula nyama yake.

Hii, alisema, itazalisha mapato ambayo yanaweza kulipa deni kubwa la nchi.