Tufahamisheni kuhusu mikutano yenu ya kisiasa- Polisi wawaambia wagombea wa Nairobi

Muhtasari

•Mungera alisema kuwa wanasiasa kutoka pande tofauti za kisiasa wanakabiliana wakati wa kampeni zao.

•Mungera alisema kuwa wako na polisi wa kutosha kuhakikisha hali ya usalama katika mikutano ya kisiasa.

Bosi wa Polisi jijini Nairobi James Mugera
Bosi wa Polisi jijini Nairobi James Mugera
Image: MAKTABA

Polisi katika kaunti ya Nairobi sasa wanawarai wanasiasa kuwafamisha kuhusu mipango yao ya mikutano ya kisiasa ili waweze kupata ulinzi wa kutosha wakati wa kampeni zao.

Kamanda ya polisi kaunti ya Nairobi Bw. James Mungera alisema kuwa wanasiasa kutoka pande tofauti za kisiasa wanakabiliana wakati wa kampeni zao, jambo ambalo husababisha machafuko yanayopelekea hasara.

 Alisema kuwa waandalizi wa mikutano ndio waonafaa kuhakikisha kuna usalama wa kutosha wakati wa kampeni.

Mugera alitoa mfano ya mkutano uliofanyika Embakasi Mashariki, ambapo wafuasi wa Mbunge Babu Owino na Micheal Ogada walikabiliana vibaya.

Waliweza kuwakamata wafuasi wawili wa mmoja wa wanasiasa hao na  kuwapata na silaha

‘Washukiwa wawili  walikua katika mstari wa mbele  wa mapigano hayo, tunatafuta zaidi’alisema.

Kampeni zimeshika kasi kwa ajili ya uchaguzi ya Agosti tarehe 9 mwaka huu.

‘Usalama ni kitu muhimu wakati wa kampeni na lazima tushirikiane kuhakikisha kuwa kuna usalama. Chukua  muda wako kuwafahamisha polisi kuhusu hayo.”

Polisi wamesema uchunguzi wao umebaini kuwa visa kama hivyo vimeripotiwa  katika maeneo bunge mengine kadhaa kama vile  Ruaraka, Mthare, Kasarani na Roysambu.

Mungera alisema kuwa wako na polisi wa kutosha kuhakikisha hali ya usalama katika mikutano ya kisiasa

Idara ya polisi imekatiza likizo ya baadhi ya maafisa na vile vile kuwahamisha katika vituo tofauti tofauti hapa nchini ili kuhakikisha uwepo wa usalama wa kutosha wakati ya uchaguzi

Naibu Inspekta generali ya Polisi Edward Mbugua aliagiza kukatizwa kwa uhamisho kupitia Ilani ya ndani mnamo Julai 3.

‘Maafisa ambao wamehamishwa kutoka vituo vyao wasitoke  mpaka uchaguzi mkuu ukamilike’ alisema

Alisema kuwa uhamisho wao utasalia jinsi ilivyo pangwa lakini wakati wakuhama vituo ndio utakaotekelezwa baada ya uchaguzi.

Hii imezingatiwa kwa mnajili ya kupanga hali ya usalama hapa nchini Kenya.