Uhuru anatumia sera ya ardhi iliyoteketezwa kuunda serikali ijayo-Adai Mudavadi

Muhtasari
  • Mudavadi alidai Uhuru alikuwa akitumia "sera ya ardhi iliyoungua" anapojiandaa kuondoka ofisini
Kinara wa ANC Musalia Mudavadi (Kulia) akihutubia wananchi wa Busia akiwa na kiongozi wa Ford Kenya Moses Wetangula.
Kinara wa ANC Musalia Mudavadi (Kulia) akihutubia wananchi wa Busia akiwa na kiongozi wa Ford Kenya Moses Wetangula.
Image: @WilliamsRuto/Twitter

Kiongozi wa chama cha ANC Musalia Mudavadi amemkashifu Rais Uhuru kwa kupanga njama ya kufanya iwe vigumu kwa Naibu Rais William Ruto kuongoza serikali iwapo atashinda uchaguzi.

Mudavadi alidai Uhuru alikuwa akitumia "sera ya ardhi iliyoungua" anapojiandaa kuondoka ofisini.

Sera ya ardhi iliyochomwa ni mkakati wa kijeshi ambao unalenga kuharibu kitu chochote ambacho kinaweza kuwa na manufaa kwa adui.

Mali yoyote ambayo inaweza kutumiwa na adui inaweza kulengwa, ambayo kwa kawaida inajumuisha silaha, magari ya usafiri, tovuti za mawasiliano na rasilimali za viwanda.

“Rais Uhuru Kenyatta anatumia sera ya ardhi iliyoteketezwa kuunda serikali ijayo kwa kushindwa. Huu ndio mchezo anaocheza,” alisema.

Akihutubia wafuasi wake katika uwanja wake wa Vihiga siku ya Alhamisi, kiongozi huyo wa ANC alisema Kenya Kwanza inafahamu vyema njama ya Uhuru na iko tayari kukabiliana na hali yoyote itakayotokea.

Kama Kenya Kwanza tuko imara. Tuna kile kinachohitajika. Tunao wataalam ambao watatusaidia kuitoa nchi katika hali mbaya ya kiuchumi,” aliongeza.

"Wakiondoka, watakuwa wakiweka sumu kwenye visima vya maji ili Kenya Kwanza itakapochukua mamlaka, tukuta nchi ina matatizo mengi ya kushughulikia."

Mudavadi aliongeza kuwa utawala wa sasa unafanya kama alivyofanya Rais wa zamani wa Iraq Saddam Hussein alipokuwa akiondoka katika nchi jirani ya Kuwait baada ya uvamizi.