'Huu sio wakati wa vurugu,'NCIC yawaonya wanasiasa huku ikilaani vikali ghasia za Jacaranda

Muhtasari
  • Tume hiyo hata hivyo imesema kwamba imeanzisha uchunguzi,ili kuwakamata waliohusika katika vurugu hivyo
Image: NCIC/TWITTER

Tume ya Kitaifa ya Uwiano na Utangamano (NCIC) imelaani vurugu viliyofanyika Jumapili tarehe 19 Juni 2022 katika uwanja wa Jacaranda jijini Nairobi.

Tume hiyo hata hivyo imesema kwamba imeanzisha uchunguzi,ili kuwakamata waliohusika katika vurugu hivyo.

"Kama Tume iliyopewa jukumu la kuwezesha kuishi pamoja kwa amani, tumezindua uchunguzi, na hivi karibuni tutawakamata wale waliohusika katika kuandaa na kutekeleza vurugu,"Ilisoma taarifa ya NCIC siku ya Jumatatu.

Aidha iliwaonya wanasiasa dhidi ya kutekeleza vurugu, huku ikisema kwamba huuu sio wakati wa vurugu kama nchi,inapoelekea katika uchaguzi mkuu wa Agosti.

"Kwa hili tunatoa taarifa kwa wanasiasa kwamba huu si wakati wa vurugu kama njia ya kufanya uhamasishaji wa kisiasa. Kama nchi na kama NCIC, tunasalia kujitolea kufikia maadili ya kisiasa katika uchaguzi mkuu wa 2022. Hatutavumilia majambazi ya kisiasa iliyoonyeshwa kwenye kiwanja cha Jacaranda jana. Kwa ajili hiyo, tunaviomba vyama vyote vya siasa sio tu kulaani vitendo hivyo Jacaranda, lakini pia kujitolea wenyewe, wanachama na wafuasi wao kwa siasa adabu katika kipindi hiki kigumu katika nchi yetu."