logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Ulipewa kazi, umefanya nini?- Rais Kenyatta amshambulia Ruto

"Wakiona mtu na shida wanasema watatatua. Kwa nini hamkutatua mkiwa ofisini?" -Alisema

image
na Samuel Maina

Uchaguzi02 July 2022 - 11:33

Muhtasari


  • •Uhuru alisema Ruto  alikuwa na miaka minane ya kutekeleza ahadi nyingi za maendeleo anazotoa sasa lakini hakuweza.
  • •Rais aliwahimiza Wakenya kufanya maamuzi ya busara kabla ya uchaguzi wa Agosti huku akiwakumbusha mustakabali wao uko hatarini.

Rais Uhuru Kenyatta bado ameendelea kumtupia vijembe naibu wake William Ruto huku zikiwa zimesalia siku 38 tu kabla ya uchaguzi mkuu wa Agosti 9.

Akizungumza katika hafla iliyofanyika KICC Jumamosi, Rais bila kutaja jina lake, alimsuta naibu wake kwa kutoa ahadi nyingi ilhali alikuwa na fursa ya kutekeleza.

Uhuru alisema DP alikuwa na miaka minane ya kutekeleza ahadi nyingi za maendeleo anazotoa sasa lakini hakuweza.

"Nasikitika nikiona wengine huko ng'we ng'we. Mtu amepewa kazi, badala ya kazi ni mdomo, mdomo, mdomo tu. Alafu anaanza kusema tutafanya na tutafanya," alisema.

"Kwa nini haukufanya ukiwa na kazi.Hii maneno ya makelele huko, huko, watu wawache upuzi... Munya hapa amefanya kazi kwa miaka mitatu. Hao walikua miaka nane walifanya nini?"

Aliongeza:

"Wakiona mtu na shida wanasema watatatua. Kwa nini hamkutatua mkiwa ofisini?"

Rais aliendelea kuwahimiza Wakenya kufanya maamuzi ya busara kabla ya uchaguzi wa Agosti huku akiwakumbusha mustakabali wao uko hatarini.

Uhuru alibainisha kuwa hajashurutisha mtu yeyote kuunga mkono kambi fulani lakini akasema ni juu ya Wakenya kutathmini viongozi wao kabla ya kuwapigia kura.

"Lakini vile nimesema ni shauri zenu. Sijalazimisha mtu kitu nimesema mfikirie. Fikira, Fikiria, Fikiria."


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved