Ata kama nilimlazimsha Uhuru awe rais iko makosa-DP Ruto awarushia vijembe wapinzani wake

Muhtasari
  • “Mimi ndiye nilifanya kampeni kubwa, nilikuwa naamka asubuhi nikafanya mikutano tatu kabla ya kuamka, na sababu mimi niafiki yake,” aliongeza Ruto.
DP RUTO WAKATI WA MANIFESTO YA KENYA KWANZA 30 JUNI 2022
Image: EZEKIEL AMING'A

Naibu Rais William Ruto ametetea maoni yaliyotolewa kwenye kanda ya sauti iliyohusishwa naye ambapo alidaiwa kumlazimisha Rais Uhuru Kenyatta kurudia Uchaguzi Mkuu wa 2017.

Katika klipu iliyochezwa kwenye mkutano wa Azimio La Umoja Jumapili na Mbunge wa Suna Mashariki Junet Mohamed, Naibu Rais Ruto alisema baada ya kura za 2017 kubatilishwa, mshirika wake katika kinyang'anyiro hicho, Rais Kenyatta, nusura aache kinyang'anyiro hicho.

DP, katika klipu hiyo, alisema Uhuru hata alimwambia kwamba anarejea nyumbani kwake kijijini Ichaweri, kaunti ya Kiambu, ambapo, "ingekuwa si kwa heshima," nusura ampige makofi Bw. Kenyatta.

Kanda hiyo iliwafanya wanasiasa wanaomuunga mkono kiongozi wa Azimio Raila Odinga kumgeukia DP Ruto, wakimtuhumu kuhusika na mgogoro wake na rais.

“Sahau kuhusu unafiki. Sahii wanajifanya wanamtetea Uhuru, hamjawahi kumpigia kura , hamjui tulifanya vipi ndio Uhuru awe Rais. Huna kazi ya kutupa mihadhara kuhusu uhusiano wetu na Uhuru Kenyatta. Tulimfanya rais kupitia kampeni na kura zetu,” DP aliwaambia wapinzani.

“Kwani mlitaka tucheze na kiti alichokuwa amepata na tumeamka saa kumi kutafuta kura? Hata kama nilimlazimisha awe rais, ni makosa?” aliuliza Ruto.

Ruto aliongeza kuwa alijitahidi sana kupata uungwaji mkono kwa azma yake ya urais na Bw Kenyatta kuona inazama.

Wamerecord oh, William Ruto amelazimisha Rais, vile [Former Chief Justice David] Maraga amebatilisha uchaguzi ukitaka tucheze, hata mngekuwa mimi, mngekubali awache na tumemtafutia?”

“Mimi ndiye nilifanya kampeni kubwa, nilikuwa naamka asubuhi nikafanya mikutano tatu kabla ya kuamka, na sababu mimi niafiki yake,” aliongeza Ruto.

“Niwaulize, si sisi tulioamka na kujitokeza kwa wingi kama mchwa kumpigia kura Rais Kenyatta. Ulitaka nimruhusu Uhuru Kenyatta amwachie Raila Odinga nafasi hiyo? Hata nikimlazimisha Uhuru kuwa rais, nilifanya makosa? Ni rafiki yangu,” Ruto alisema.