(Video) "Raila hana makaratasi ni kama mimi, tuko wengi" - Oscar Sudi

Sudi alidai kwamba anahangaishwa bure juu ya vyeti hali ya kuwa wako kwenye ligi moja na Raila ambaye pia hana.

Muhtasari

• Mbunge huyo alisema katika wanasiasa wote anaamini tu Moses Wetangula ndiye pekee mwenye vyeti halali kutokana na ubora wake katika lugha ya kiingereza.

Mbunge wa Kapseret Oscar Sudi amelisukuma gumzo la wanasiasa wengi kukosa vyeti halali mbele kwa kujitetea kwamba kumbe walikuwa wanamkimbiza na kumhangaisha hali ya kuwa wako wengi.

Katika mkanda wa video moja ambayo aliipakia kwenye ukurasa wake wa Twiiter wikendi iliyopita, Sudi alionekana kuwa na furaha ya kupata wanachama wanaohangaishwa na ukosefu wav yeti halali vinavyoonesha jinsi walipata masomo yao.

“Si mnaona hawa watu wananikimbiza eti sikusoma, lakini si mmeona wale watu hawajasoma ni weingi, wengi sana, lakini Mungu amefungua barabara,” Sudi anaonekana akisema huku umati ukimsherehekea.

Mbunge huyo aliendelea kusema kwamba wapo wanasiasa wengi tu ambao hawana vyeti tu kama yeye ila suala lao limefumbiwa macho kwa sababu wanatetewa na vyombo wad ola. Sudi aliahidi kwamba kuna baadhi ya viongozi watachunguzwa uhalali wav yeti vyao kama ambavyo yeye anachunguzwa.

“Si mnajua Tinga (Raila) hana makaratasi ni kama mimi, si mnajua Gideon (Moi) hana makaratasi ni kama mimi. Si mnajua hata hii akina Joho hili kundi lote hili, hata ya Uhuru tutachunguza. Wanaanza kusema sijui Sakaja hana, sijui nani hana. Sasa hata hatujui nani hana,” Sudi alisema.

Mbunge huyo alizidi kujitetea kwamba wako wengi wasiokuwa na vyeti halali lakini kwa bahati mbayqa ni yeye tu amekuwa akiteswa kortini.

“Si mmeona tu hawa watu wamekuwa wakinitesa mimi pekee kortini kumbe hata Tinga mwenyewe ni bure. Ukikuja hawa watu wengine ni bure, sasa wenye wako na makaratasi ni wachache sana hata mimi nitaanza uchunguzi,” alisema Sudi kwa maskitiko makubwa.

Alisema kwamba kwa wanasiasa ambao anaweza wakubali uhalali wav yeti vyao ni seneta wa Bungoma Moses Wetangula kutokana na weledi wake katika lugha ya kiingereza.

Akionekana kujitetea, Sudi alisema kwamba si eti hana makaratasi bali ni vile siasa imeingizwa katika kuchunguzwa kwa makaratasi yake na kuuliza umati kama kweli wanaona yeye anakaa mtu hakuenda shule.

“Hebu nikiwauliza nyinyi walunje, mkiniona vizuri vile nimesimama, na vile mmekuja hapa na vile mmenipima, mimi nakaa mtu sikuenda shule? Mimi nakaa mtu bandia? Si mimi niko mbele, si mimi nashinda hata hao maprofesa?” Alisema Oscar Sudi huku akiaga jukwaa kwa kushangiliwa na umati.