EACC yawaonya Wakenya dhidi ya haya wakati wa uchaguzi mkuu

Tume hiyo imeeleza kuwa wananchi ndio watapata madhara ya uongozi usio na maadili katika uchaguzi wowote.

Muhtasari
  • EACC yawaonya Wakenya dhidi ya haya wakati wa uchaguzi mkuu
Image: HISANI

Huku zikiwa zimesalia siku 30 pekee hadi uchaguzi mkuu wa Agosti , tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi imewaonya Wakenya kuepuka hongo wakati wa uchaguzi.

Katika taarifa iliyotolewa na tume hiyo Jumamosi tarehe 9 Julai, Wakenya hasa vijana wameonywa kuhusu hatari ya kuwachagua viongozi kwa sababu ya kuhongwa.

Tume hiyo imeeleza kuwa wananchi ndio watapata madhara ya uongozi usio na maadili katika uchaguzi wowote.

"MUONGOZO WA WAPIGA KURA 2022: Wananchi, hasa VIJANA, wanapaswa KUKATAA RUSHWA YA WAPIGA KURA na kutoa maamuzi ya upigaji kura kwa kuzingatia uadilifu na umahiri wa wagombea. Hatimaye, ni wananchi kuteseka. matokeo ya uongozi usio na maadili katika ofisi yoyote ya uchaguzi" taarifa hiyo inasomeka.

Wakenya wamepewa changamoto ya kuchagua kubadilishana shilingi mia tano na uongozi duni wa miaka mitano au kukataa hongo na kupata viongozi ambao watakuwa msaada kwao katika kuleta maendeleo katika miaka mitano ijayo.