Raila amkashifu Ruto kwa kumlaumu kuhusu kupanda kwa bei ya unga

Raila alizungumza Ijumaa wakati wa mkutano wa kampeni huko Lugari, kaunti ya Kakamega.

Muhtasari
  • Raila alimtupia lawama Naibu Rais akisema aliwezesha uagizaji wa mahindi na kusababisha bei ya juu ya unga nchini
KInara wa ODM Raila Odinga
Image: George Owiti

Mgombea urais wa Azimio Raila Odinga sasa anasema ni upuuzi kwa mpinzani wake wa Kenya Kwanza William Ruto kumlaumu kwa kupanda kwa bei ya unga.

Raila alimtupia lawama Naibu Rais akisema aliwezesha uagizaji wa mahindi na kusababisha bei ya juu ya unga nchini.

"Unajua wamekuwa wakilalamika kuwa gharama ya maisha ni kubwa...Waulize walioleta mahindi kutoka Mexico. Yeye (Ruto) ndiye aliyeharibu soko la mahindi hapa," Raila alisema.

Raila alizungumza Ijumaa wakati wa mkutano wa kampeni huko Lugari, kaunti ya Kakamega.

Mnamo 2017 na 2020, serikali iliruhusu uingizaji wa mahindi kutoka Mexico ili kupunguza upungufu huku wakulima wakisubiri msimu wa mavuno.

Ruto amekuwa akimsuta kiongozi huyo wa ODM akidai handshake kati yake  na Rais Uhuru Kenyatta 2018 ndio sababu ya bei ya unga kupanda.

“Mnamo 2018, pakiti ya kilo 2 ya unga wa mahindi iligharimu Sh75. Sasa inauzwa kwa Sh250 na tunaambiwa kwamba baada ya kupigwa kiwiko, [ni] yule jamaa wa Azimio,” alisema wakati wa mkutano huko Kilifi mnamo Juni 26.

Ruto alidai Raila alikuwa akimpa Uhuru ushauri mbaya, na kusababisha gharama ya juu ya maisha kwa sasa.

Mnamo 2017, Raila alitishia kuwafichua waliohusika na uagizaji wa mahindi kutoka nje, na kudai DP ni miongoni mwa waliohusika.

Alisema utaratibu wa kuagiza mahindi kutoka nje ya nchi ulikuwa wa samaki na anashangaa imekuwaje kwa muda mfupi usafirishaji huo kufika nchini Kenya.

Matamshi yake Raila yanairi siku moja tu bada ya wakenya kutishia kususia kupiga kura mnamo Agosti iwapo bei ya bidhaa muhimu haitapunguzwa.