Ukisusia uchaguzi bado utaendelea-Wetangula amwambia Raila

Wetangula alitoa wito kwa wakazi wa Lokichar kujitokeza kwa wingi na kuipigia kura Kenya Kwanza.

Muhtasari
  • Alisema Raila alipinga utumizi wa sajili ya mwongozo mwaka wa 2017 ilhali anashinikiza hilo sasa
  • Wiki jana, Raila alisema uchaguzi haufai kufanywa ikiwa IEBC haitakuwa na sajili ya mwongozo
  • Lakini Wetangula alisema Raila katika uchaguzi uliopita alisisitiza sajili ya kielektroniki na kushangaa kilichobadilika sasa
Kiongozi wa Ford Kenya Moses Wetangula kwenye mkutano wa kisiasa katika wadi ya Soysambu eneo bunge la Tongaren.
Kiongozi wa Ford Kenya Moses Wetangula kwenye mkutano wa kisiasa katika wadi ya Soysambu eneo bunge la Tongaren.
Image: JOHN NALIANYA

Kiongozi wa Ford Kenya Moses Wetangula amethubutu Muungano wa Azimio na mgombeaji wake wa urais Raila Odinga kususia uchaguzi wa Agosti.

Akizungumza huko Lokichar katika ziara ya kampeni katika Kaunti ya Turkana, Wetangula aliambia Azimio kwamba uchaguzi bado utaendelea hata kama timu ya Raila itajiondoa.

“Tunataka kumwambia huyo mtu wa ‘vitendawili’ alete. Ukisusia uchaguzi bado utaendelea na wewe au bila wewe,” alisema.

Alisema Raila alipinga utumizi wa sajili ya mwongozo mwaka wa 2017 ilhali anashinikiza hilo sasa.

Wiki jana, Raila alisema uchaguzi haufai kufanywa ikiwa IEBC haitakuwa na sajili ya mwongozo.

Lakini Wetangula alisema Raila katika uchaguzi uliopita alisisitiza sajili ya kielektroniki na kushangaa kilichobadilika sasa.

"Ulisema serikali haiwezi kutumia mamilioni ya fedha kisha itumie mwongozo. Sasa mmefanya zamu kwamba mnataka sajili ya mw

Wetangula alitoa wito kwa wakazi wa Lokichar kujitokeza kwa wingi na kuipigia kura Kenya Kwanza.

Seneta huyo wa Bungoma aliongeza kuwa manifesto ya Kenya Kwanza itahakikisha wakazi wanapata kadi ya NHIF ili kupata matibabu katika kituo chochote.

“Tutakuwa na elimu ya bure na tukifika Chuo Kikuu, tutapata mkopo wa asilimia 100 bila riba. "alisema.