(Video) Mbunge wa Kikuyu Kimani Ichung'wa aonekana akipika chapati kwenye banda

Kimani Ichung'wa aliteuliwa kwa mara ya kwqanza kaam mbunge mwaka 2013.

Muhtasari

• Kimani Ichung'wa analenga kutetea kiti chake kwa mara ya tatu mtawalia kupitia tikiti ya chama cha UDA.

Mbunge wa Kikuyu Kimani Ichung’wah amegonga vichwa vya habari na kuzua gumzo pevu baada ya video kusambaa mitandoni akionekaan kusaidia maam ntilie mmoja kupika chapati katika kibanda.

Mbunge huyo anaonekana akielekeza weledi wake katika upishi wa chapati kwenye kibanda alikopita katika saka saka za kura huku akinadi sera zake kuelekea uchaguzi mkuu ujao siku thelathini kutoka sasa.

Wimbo wa mwanamuziki mkongwe wa Kikuyu, Kioi wa karanga Chapo unasikika ukiimba huku Ichung’wa anaonekana akijishughulisha zaidi kwa jitihada kubwa kugeuza chapati mekoni huku umati wa wafuasi wake ukimuangalia kwa mshangao mkubwa.

Ichung’wa ambaye alichaguliwa kama mbunge kwa mara ya kwanza mwaka 2013 kupitia tikiti ya chama cha Jubilee kwa sasa analenga kutetea kiti hicho chake kwa mara ya tatu mtawalia kupitia tikiti ya chama cha UDA, kinachoongozwa na Rafiki wake mkubwa naibu rais William Ruto.

Video hiyo ilisambazwa kwa mara ya kwanza na kundi fulani kweney mtandao wa Facebook linalojiita Hustlers News na imepokea maoni mbali mbali huku wengi wakisema huyo mwanasiasa anajinyenyekesha kwa wananchi wapiga kura ili kuzoa kura zao lakini pindi baada ya kukamilika kwa uchaguzi, hakuna atakayemuona.

Hiki ni kimoja kati ya visa vya kushangaza ambavyo wanasiasa wanajishughulisha navyo kwa wapiga kura kama njia moja ya kuonekana wachapa kazi ili kupigiwa kura.

“Ujinga ambao uko Kenya ni mwingi sana,,,,huyu ni mtu wa aina gani? hatakiwi kupigiwa kura. Saa hii wanajifanya hivyo wako wanyenyekevu na marafiki lakini baada ya uchaguzi hawataonekana tena,” mmoja kwa jina la Wicklife Mbinga aliandika.

Wengine walimtetea Ichung’wa kwa kusema kwamba amepigiwa kura nchini Kenya kama mbunge bora zaidi tena mchapa kazi na kwa hiyo hajaanza leo mambo yake hayo ya kutoa huduma kwa wananchi.

“Amepigiwa kura mara nyingi kama mbunge bora nchini, achene wivu. Huyu jamaa ni kiongozi kweli. Yeye na Ndidi ni wakarimu sana kwa watu wanaowaongoza,” mwingine aliandika.