Mudavadi asema Raila ni mnafiki kwa kutumia bei unga kuhadaa wakenya

Mudavadi aliwataka wakenya kuwa macho na kukataa mbinu za Azimio za kutaka kuwahadaa wakati huu

Muhtasari

• Mudavadi aliwataka wakenya kuwa macho na kukataa mbinu za Azimio za kutaka kuwahadaa wakati huu ambapo Wakenya wamesalia na siku 19 pekee kabla ya kwenda kwenye uchaguzi Agosti 9, 2022.

Kinara wa ANC Musalia Mudavadi
Kinara wa ANC Musalia Mudavadi
Image: WILFRED NYANGARESI

Kinara wa ANC Musalia Mudavadi amemkosoa vikali mgombeaji wa Urais kwa tiketi ya Muungano wa Azimio la Umoja-One Kenya Raila Odinga na kumtaja mnafiki.

Akihutubia mkutano wa kampeini mjini Nairobi siku ya Jumatano, Mudavadi alisema kuwa Raila anawahadaa wakenya kwa kupitia rais Uhuru Kenyatta  kwamba serikali imeafikia kupunguza bei ya unga kutoka zaidi ya shilingi 230 hadi shilingi 100 kwa pakiti ya kilo mbili.

Mudavadi aliwataka wakenya kuwa macho na kukataa mbinu za Azimio za kutaka kuwahadaa wakati huu ambapo Wakenya wamesalia na siku 19 pekee kabla ya kwenda kwenye uchaguzi Agosti 9, 2022.

“Sahizi mimi nataka niulize kwa kiwazi wale ambao tangu jana jamaa waseme ati bei ya Unga imeshuka hadi shilingi 100, mimi nataka niulize kuna mtu yeyote hapa ambaye ameenda kwa duka na amepata unga kwa bei ya shilingi 100,” Mudavadi alisema.

Mudavadi akiweka wazi kuwa Serikali kupitia wizara ya Kilimo huenda haijafikiana na makampuni ya kusaga unga wa mahindi na hivyo basi taarifa kwamba bei ya unga ingeshuka ni za kuwahadaa tu wananchi.

Akirejelea usemi wa Kinara wa ODM Raila Odinga akiwa Gilgil, alipoelezea nchi kwamba alikuwa amezungumza na rais Uhuru Kenyatta na kuafikiana kwamba bei ya Unga ishuke hadi shilingi mia moja, Mudavadi alitilia shaka usemi huu wa Raila.

Alisema sio tu rahisi kwa Raila kuafikiana na wafanyibiashara katika sekta ya mahindi bila utaratibu mwafaka kufuata.

“Hawa majama ni wajanja sana. Huu ndio ujanja wa hii serikali kwasababu hawa majamaa wanadanganya kwamba wameafikiana na wasagaji , na ukweli wa mambo ni kwamba kama msagaji alikuwa ashanunua mahindi yake kwa bei fulani, amesaga na kisha ame sambaza kwa maduka kulingana na bei ya ununuzi, utamlazmisiha aje arudishe bei chini nay eye pia ametumia hiyo gharama yake. Huu ndio uwongo wa hawa majamaa,”  alisema Mudavadi.

Mudavadi sasa ameilimbikizia lawama serikali kwa kuwapuuza wakulima na kutowajibikia uboreshaji wa kilimo kupitia kuwapiga jeki wakulima hasa wale wa mahindi kwa kuwapa mbolea na pembejeo kwa bei nafuu na vile vile kuboresha bei ya mauzo ya zao hili.  Alisema kuwa hii ni mojawepo ya sababu kuu zilizopelekea taifa kukumbwa na uhaba wa mahindi na hivyo basi ongezeko la bei ya Unga kushuhudia pasi na masihara mengine yaliyochangiwa na serikali ya Rais Uhuru Kenyatta na kupelekea gharama ya maisha kuwa ghali mno nchini.

“Yale madeni hawa majamaa wametuachia yanahitaji serikali ambayo itaelewa mambo ya uchumi. We are in very serious trouble because of these fellows, but there is hope and that hope is in Kenya Kwanza. Tunataka ajira ipatikane, tunataka wafanyibiashara wanawiri, tunataka wakulima wawe saw ana Watoto wetu wasome kwa njia iliyo sawa. I can tell you there is no other political organization that has the right agenda for Kenya other than Kenya Kwanza. Na mkiona huyu Sakaja hapa on a serious note, don’t you see someone who is ready to serve Nairobians and Kenyans? Naomba tumusaidie,” Mudavdi alisema.

Siku ya Jumatano Mudavadi alizuru maeneo kadhaa ya jiji Nairobi kwenye kampeni za Kenya Kwanza.