logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Hatimaye Raila aweka wazi hatoshiriki mdahalo wa urais, "Siwezi shiriki meza moja na Ruto"

Mwakilishi wa kamati ya kampeni za Raila, profesa Makau Mutua alisema Raila kushiriki mdahalo huo ni kama kumsaidia Ruto kunadi sera zake.

image
na Radio Jambo

Habari24 July 2022 - 08:47

Muhtasari


• "Sisi tumekubali hatutasaidia kuwezesha kampeni zake kwani Raila kushiriki ni kama njia moja ya kumsaidia Ruto kunadi sera zake" - Makau Mutua

Hatimaye mpeperusha bendera wa muungano wa Azimio la Umoja One Kenya, Raila Odinga ameweka wazi kwamba hatoshiriki kwenye mdahalo wa urais uliokuwa umeratibiwa Jumanne wiki hii kwa kile alisema kwamba hatoweza kushiriki meza moja na mpeperusha bendera wa muungano wa Kenya Kwanza, William Ruto.

Katika taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari Jumapili, mwakilishi wa kamati ya kampeni za Raila msomi profesa Makau Mutua alisema kwamba William Ruto ambaye alikuwa anatarajiwa kumenyana na Raila kwenye mmdahalo huo hana vigezo vya kugombea na hivyo Raila kushiriki ni kama kujichafulia jina.

“Yatakuwa ni makosa makubwa mno kumzawidi mtu kama huyo kwa mdahalo wa kitaifa. Sisi tumekubali hatutasaidia kuwezesha kampeni zake kwani Raila kushiriki ni kama njia moja ya kumsaidia Ruto kunadi sera zake. Acha ajieleze mwenyewe na sera zake potovu kwa wananchi bila usaidizi wetu,” Makau Mutua alisema.

Taarifa hiyo ilisema kwamba badala ya Raila kuhudhuria mdahalo huo ,ataandaa mkutano wa wananchi katika ukumbi wa kijamii wa Jericho ili kushiri,I na wananchi kuwasikiliza maoni yao. Mkutano huo wake utaoneshwa kwenye runinga.

Raila kususia mdahalo huo inakuja siku chache tu baada ya mgombea urais wa chama cha Roots, wakili msomi George Wajackoyah kusema kwamba hata yeye hatashiriki mdahalo huo kama hawatakuwa meza moja na wagombea wengine watatu, David Mwaure wa Agano, Raila Odinga wa Azimio na William Ruto wa Kenya Kwanza.

Madai ya Raila kulenga kukwepa mdahalo huo yalianza kusemwa na katibu wa mawasiliano katika kamati ya kampeni zake Dennis Onyango ambaye alifokea jinsi mdahalo wa wagombea wenza ulivyoendeshwa na kusema kama ndio hivyo basi watu wasiwe na matumaini makubwa sana kama Raila atashiriki.

Ijumaa wiki jana mbunge wa Suna Mashariki, Junet Mohammed katika mkutano wa kisiasa kwenye kaunti ya Trans Nzoia pia alisema Raila hangeshiriki mdahalo huo kama masuala ya ufisadi, uongozi na uadilifu hayatapewa kipaumbele. Badala yake, alisema muungano huo utamtuma mbunge Babu Owino kumwakilisha Baba.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved