ODM yamteua aliyekuwa msanii wa Sol-Generation Crystal Asige kwenye seneti

Mwimbaji huyo ameteuliwa kuwakilisha watu wanaoishi na ulemavu.

Muhtasari

•Asige ameteuliwa na chama cha ODM katika seneti pamoja na mwenzake wa kiume Kakiri Ochieng. 

•Crystal alijipatia umaarufu kama mwanamke wa kwanza kwenye lebo ya kwanza ya sol Generation.  

Msanii Crystal Asige
Image: MAKTABA

Chama cha Orange Democratic Movement (ODM) kimemteua aliyekuwa msanii wa Sol Generation, Crystal Asige kwenye Seneti. 

Katika orodha ya uteuzi iliyochapishwa na Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) Jumatano,  mwimbaji huyo ameteuliwa kuwakilisha watu wanaoishi na ulemavu. 

Asige, ambaye ni mwanachama wa zamani wa Sol Generation, ameteuliwa na ODM katika seneti pamoja na mwenzake wa kiume Kakiri Ochieng.

Crystal alijipatia umaarufu kama mwanamke wa kwanza kwenye lebo ya kwanza ya sol Generation.  

Baadaye alitengana na Sauti Sol mnamo 2019 katika hali isiyoeleweka. 

Msanii huyo mwenye ulemavu wa macho amekuwa akizungumzia changamoto za watu wanaoishi na ulemavu na kueleza maisha yake ya kisanii kupitia muziki wake.