Chebukati na DCI watatua tofauti zao kuhusiana na stika za IEBC

Chebukati alisema taasisi hizo mbili zitaendelea kushirikiana katika maandalizi ya uchaguzi

Muhtasari

• IEBC na polisi waliahidi kushirikiana kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa njia huru na yenye uazi bila vurugu.

Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) na idara ya polisi wametatua tofauti zao zilizotokana na sakata ya kuzuiliwa kwa stika za tume ya uchaguzi zilizonaswa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA). 

Kulingana na Inspekta Jenerali wa Polisi Hillary Mutyambai, hii ilifuatia mkutano wa mashauriano na Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati siku ya Alhamisi. 

Kwa upande wake, Chebukati alisema kuwa taasisi hizo mbili zitaendelea kushirikiana katika maandalizi ya uchaguzi ili kuhakikisha kuwa kunafanyika uchaguzi huru na wenye haki usiokuwa na vurugu.