Raila aimarisha uongozi wake mbele ya Ruto kwa 47%, Ruto 41% - IPSOS

George Wajackoyah angeibuka wa tatu kwa asilimia 2.9 huku David Mwaure wa Chama cha Agano akipata asilimia 0.2.

Muhtasari

• Utafiti huo uliofanywa kati ya tarehe 23 - 26 Julai una asilimia 4 ya wapiga kura ambao hawajaamua ambao wanaweza kutikisa kinyang'anyiro hicho. 

Kinara wa ODM Raila Odinga na Kinara wa UDA William Ruto
Kinara wa ODM Raila Odinga na Kinara wa UDA William Ruto
Image: Maktaba

Mgombea urais wa Azimio Raila Odinga anasalia kuwa kipenzi cha Wakenya kwa wadhifa wa urais siku sita kabla ya uchaguzi, hii ni kulingana na kura ya maoni ya Ipsos. 

Kura hiyo iliyotolewa siku ya Jumanne inaonyesha kwamba Raila atashinda asilimia 47 ya kura zote akimshinda mpinzani wake mkuu Williams Ruto aliyepata asilimia 41. 

Kiongozi wa Chama cha Roots George Wajackoyah angeibuka wa tatu kwa asilimia 2.9 ya kura huku David Mwaure wa Chama cha Agano akipata asilimia 0.2. 

Kwa hitilafu ya ukingo ya asilimia +/-1.25, hakuna mgombea ambaye angeweza kutangazwa mshindi katika mkondo wa kwanza kwani hakuna anyefikisha zaidi ya asilimia 50 kama inavyotakikana katika katiba. 

Hata hivyo, utafiti huo uliofanywa kati ya tarehe 23 - 26 Julai una asilimia 4 ya wapiga kura ambao hawajaamua ambao wanaweza kutikisa kinyang'anyiro hicho. 

Utafiti huo ulikuwa na wahojiwa 6,105 kutoka kaunti zote 47.