logo

NOW ON AIR

Listen in Live

(+Video) Raila amuonya Arati dhidi ya kuvurugana na gavana Ongwae Kisii "Heshimu wazee!"

:Sasa mimi namwambia Arati kama anawania ugavana, awanie lakini aheshimu wengine. Nimemwambia asiite watu wengine wezi kama hawajashtakiwa na kupatikana na hatia,” Raila alizungumza

image
na Radio Jambo

Habari03 August 2022 - 08:09

Muhtasari


• Simba Arati analenga kuwa gavana wa Kisii kupitia chama cha ODM  kumrithi gavana wa sasa wa ODM, James Ongwae.

Katika kaunti ya Kisii kwa muda mrefu kipindi hiki cha kampeni kumekuwa na vurugu baina ya wanachama wa ODM, huku gavana anayeondoka James Ongwae akitofautiana wazi na mgombea ugavana Simba Arati ambao wote wako katika mwavuli wa ODM.

Ongwae amekuwa akimshtumu Arati kwa kutokuwa na heshima kwa wazee huku akiwataka wakaazi kutompigia kura Arati kuwa mrithi wake na badala yake kuwachagua wengine kama Chris Obure wa Jubilee ama seneta wa sasa profesa Sam Ongeri anayewania ugavana kwa DAP-K.

Tofauti hizi kati ya Arati na Ongwae zimemfikia kinara wa chama Raila Odinga ambaye Jumanne wakati wa hafla ya kisiasa kwenye kaunti hiyo yenye utajiri wan dizi alimuonya vikali Simba Arati na kumtaka kufanya kampeni zake kwa njia inayofaa bila kuwapeza wazee na viongozi wengine aliowapata kule baada ya kuondoka Nairobi alikohudumu kama mbunge wa Dagoretti Kaskazini kwa miaka 10.

“Huyu Simba Arati tumetoka na yeye mbali sana. Sasa mimi namwambia kama anawania ugavana, awanie lakini aheshimu wengine. Nimemwambia asiite watu wengine wezi kama hawajashtakiwa na kupatikana na hatia,” Raila alizungumza huku akiwa amesimama jukwaani na Simba Arati.

Alizidi kumwambia Arati kwamba anafaa kuwaheshimu wazee ili kupata baraka za uongozi kutoka kwao.

“Heshima si utumwa. Mimi namuonya kaka baba yake. Mpaka upatie wazee heshima maanake unahitaji mate yao,” Raila Odinga alitoa wosia kwa Arati.

Tafiti za hivi karibuni zinamuweka Arati wa ODM kifua mbele katika mbio za kuelekea ofosi ya gavana Kisii huku akifuatwa kwa umbali na mbunge wa Nyaribari Masaba, Ezekiel Machogu ambaye anawania ugavana kwa tikiti ya chama cha UDA.

Wengine wanaolenga kumrithi gavana Ongwae ni pamoja na Chris Obure wa Jubilee, Sam Ongeri wa DAP-K, Manson Oyongo Nyamweya wa KNC miongoni mwa wengine.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved