"Jua tu uko upinzani" Winnie Odinga ambia viongozi wa Kenya Kwanza

Winnie Odinga kudai kwamba Naibu rais akuwe tayari kuwa kiongozi wa upinzani

Muhtasari

•Kupitia ukurasa wake wa  Twitter, Winnie alisema kutokana na  mkutano wa Naibu rais na wanahabari inaonyesha kuwa yeye ndiye atakuwa kiongozi wa Upinzani baada ya uchanguzi.

Winnie Odinga
Winnie Odinga

Binti wa kiongozi wa ODM Raila Odinga, Winnie amemkejeli mgombea urais wa Muungano wa Kenya Kwanza William Ruto kwa kuitaita waandishi wa habari nyumbani kwake Karen kila mara.

Mnamo Alhamisi, Agosti 4, Ruto alihutubia wanahabari ambapo aliibua masuala kadha wa kadha, miongoni mwao akilalamika kuwa serikali inapanga kuingilia uchaguzi kupitia machifu.

DP pia alilalamika kwamba serikali ilikuwa inahujumu kampeni zake kwa kumfungia yeye na wafuasi wake nje ya maeneo, kwa mfano, uwanja wa Bukhungu na Tononoka.

Kupitia ukurasa wake wa  Twitter, Winnie alisema kutokana na  mkutano wa Naibu rais na wanahabari inaonyesha kuwa yeye ndiye atakuwa kiongozi wa Upinzani baada ya uchanguzi.

Hii ina maana kwamba Naibu rais atashindwa na mgombea urais wa Azimio la Umoja One Kenya Raila katika uchaguzi wa urais unaotarajiwa baada ya siku nne.

''Kwa uzoefu wangu, ukianza ma pressers, ujue tu uko upinzani ,Ukianza kuita press conferences, jua tu uko upinzani," Winnie alisema.

Alikuwa akirejelea mwanamkakati wa vyombo vya habari Pauline Njoroge ambaye alibainisha kuwa Ruto alianza kuwaita waandishi wa habari jinsi ODM walivyofanya kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2017.

"Waandishi wanahabari  wameanza kuitwa. Rafiki zangu wazuri wa ODM, si waambie kwamba nyinyi pia mlikuwa hivyo hivyo 2017, pia mlifanya mkutano mengi na waandishi wa habari," alisema Njoroge

Mnamo 2017, kama vile Ruto, wakati huo Raila,akiwa chini ya Muungano wa National Super Alliance (NASA), alifanya mikutano kadhaa na wanahabari akishutumu serikali kwa vitisho.