Ekuru Akukot: Ubashiri Wangu - Wakenya Watakataa Mradi wa rais Kenyatta

Aukot aliwataka Wakenya kujjitokeza na kupiga kura

Muhtasari

“Utabiri wangu: Wakenya leo watakataa mradi wa Uhuru Kenyatta" alisema Aukot.

Kinara wa chama cha Third Way Alliance, Ekuru Aukot
Kinara wa chama cha Third Way Alliance, Ekuru Aukot
Image: Twitter//EkuruAkukot

Kiongozi wa chama cha Third Way Alliance, Ekuru Aukot ameibua madai kwamba ubashiri wake katika uchaguzi mkuu wa leo Wakenya watapata nafasi ya kuukataa na kuutupiia mbali mradi wa rais anayeondoka Uhuru Kenyatta.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Aukot alisema kwamba wakenya wataukomesha mradi wa Uhuru Kenyatta pamoja na kutokomeza njama ya kile alikitaja kuwa ni kutaka kurejea madarakani kwa muhula wa tatu kupitia mlango wa nyuma.

Mwanasiasa huyo maarufu kwa msawada wa ‘Punguza Mzigo’ aliwahimiza wakenya kujitokeza kwa wingi kupiga kura huku akisisitiza kuhusu msimamo wake na kile kilichoonekana kama ako nyuma ya Wagombea urais Wengine isipokuwa yule wa muungano wa Azimio La Umoja One Kenya, Raila Odinga.

“Utabiri wangu: Wakenya leo watakataa mradi wa Uhuru Kenyatta na jaribio lake la kutaka kugombea urais wa muhula wa tatu kupitia mlango wa nyuma. Tupige kura,” Ekuru Aukot aliandika.

Aukot alikuwa miongoni mwa wanasiasa zaidi arubaini waliotangaza azma yao ya kuwania urais baada ya kukumbwa na shoka la tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC iliyomfungia nje ya kinyang’anyiro hicho kwa kutoafikia vigezo vilivyohitajika ikiwemo kuwa na Saini za wapiga kura elfu 48 pamoja na chapa za vitambulisho vya kila mmoja.

Aukot alielekea mahakamani kupinga hatua ya IEBC kumfungia nje ila uamuzi wa awali wa tume hiyo inayoongozwa na Wafula Chebukatu ukadumishwa na hivyo kumfungia nje ambapo wanne waliponea kutemwa nje.

Uchaguzi wa Jumanne Agosti 9 unafanyika na wagombea katika nyadhifa ya urais ni pamoja na David Mwaure kutoka chama cha Agano, wakili msomi George Wajackoyah wa chama cha Roots, Raila Odinga wa Azimio na William Ruto wa UDA.