"Hakuna Silaha Dhidi Yetu Itafanikiwa!" Mkewe Wajackoyah Amtia Moyo Kwa Kutopiga Kura

Miller Lee Chatham, alimtia moyo mumewe kwa mstari wa Biblia baada kufadhaika kwa kutopiga kura.

Muhtasari

• Wakati wa mahojiano ya awali ya TV, Wajackoyah aliwahi sema mkewe anaishi Marekani huku watoto wao watatu - binti wawili na kijana  mmoja wakiishi Marekani.

Meller Luchiri akiandamana na mumewe George Wajackoyah mnamo Julai 26, 2022.
Meller Luchiri akiandamana na mumewe George Wajackoyah mnamo Julai 26, 2022.
Image: EZEKIEL AMING'A

Mkewe Mgombea Urais wa chama cha Roots wakili msomi George Wajackoyah Mmarekani Meller Luchiri amemtia moyo mumewe baada ya kushindwa kupiga kura kutokana na mtambo wa kidijitali wa KIEMS kufeli na kushindwa kuwatambua wapiga kura.

Mgombea huyo wa urais mwenye ufuasi mkubwa miongoni mwa vijana Wakenya hakuweza kupiga kura baada ya kuwasili katika Shule ya Msingi ya Indangalasia huko Matungu baada ya mtambo huo wa kuwatambua wapiga kura kufeli kufanya kazi.

Akizungumza na wanahabari waliotaka kusikia hisia zake baada ya kushindwa kupiga kura, Wajackoyah alimshtumu mwenyekiti wa tume ya uchaguzi na mipaka IEBC kwa kukanganya mambo na kusema kwamba angepewa nafasi maafisa kama hao wanaosimamia uchaguzi atawafuta kazi bila kupepesa jicho.

 Katika mkutano huo na wahabahari, mke wake mrembo Mmarekani, Miller Lee Chatham, alimtia moyo mumewe kwa mstari wa Biblia baada kufadhaika kwa kutopiga kura.

"Hata hivyo, hakuna silaha itakayoundwa dhidi yetu, watu wa Kenya itafanikiwa. Huo ndio uwanja ambao tunasimama. Tuwe watulivu na tutakuwa hapa, hadi mwisho," mkewe Wajackoyah alizungumza kwa lafudhi ya kimombo kilichoonekana kuwavutia wakenya wengi waliokuwa wametamauka katika kituo hicho cha kupiga kura.

Wakati wa mahojiano ya awali ya TV, Wajackoyah aliwahi sema mkewe anaishi Marekani huku watoto wao watatu - binti wawili na kijana  mmoja wakiishi Marekani.

Mtoto wa kwanza wa kiume anaitwa Ty Luchiri, na binti zake Marjorie Luchiri na mzaliwa wa mwisho Marz Luchiri.

Wajackoyah na Meller, Mmarekani mwenye asili ya Kiafrika, walioana mapema miaka ya 90