• Kamanda wa Polisi wa Kaunti ya Nakuru Peter Mwanzo alisema mbunge huyo alimvamia na kumjeruhi mpiga kura katika kituo cha kupigia kura katika eneo bunge lake.
• Gikaria anatetea kiti chake chini ya Chama cha United Democratic Alliance (UDA).
Mbunge wa Nakuru Mjini Mashariki David Gikaria alikamatwa Jumanne kwa madai ya kushambuliwa katika kituo cha kupigia kura.
Kamanda wa polisi kaunti ya Nakuru Peter Mwanzo alisema mbunge huyo alimvamia na kumjeruhi mpiga kura katika kituo cha kupigia kura katika eneo bunge lake.
Alisema Gikaria alikamatwa katika kituo cha kupigia kura cha Shule ya Msingi ya Naka kufuatia mzozo uliovuta hisia za polisi.
"Kuna madai kwamba alimjeruhi mpiga kura na kusababisha ghasia na fujo katika kituo cha kupigia kura," Mwanzo alisema.
Alisema mpiga kura aliyevamiwa alilazwa hospitalini baada ya kupata majeraha kichwani.
Wafuasi wa Gikaria walisema alizuiliwa katika Kituo Kikuu cha Polisi cha Nakuru na kuna uwezekano akazuiliwa humo akisubiri mazungumzo ya dhamana.
Mbunge huyo si mgeni katika mabishano mjini.
Mnamo Juni, 2022 mbunge huyo alihojiwa na maafisa kutoka Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI) mjini Nakuru kuhusu uhusiano wake unaoshukiwa kuwa na genge la uhalifu.
Mnamo 2020, alikamatwa pia kwa maandamano ya matatu.
Tafsiri na MOSES SAGWE