Mwanamume akamatwa na panga,kisu katika kituo cha kupigia kura cha Homa Bay

Alikamatwa wakati polisi walipokuwa wakisafisha kituo cha kupigia kura baada ya shughuli ya kupiga kura.

Muhtasari
  • Maafisa hao walimfunga pingu mshukiwa na kumwamuru alale chini, ambapo walimkuta akiwa na silaha hizo ghafi

Mwanamume mmoja alikamatwa Jumanne katika shule ya msingi ya Shauri Yako, kituo cha kupigia kura huko Homa bay, baada ya kupatikana na panga na kisu.

Katika video iliyosambaa mitandaoni, mwanamume huyo anaonekana akiwa amefungwa pingu na kuketi chini huku polisi wakimzunguka.

Alikamatwa wakati polisi walipokuwa wakisafisha kituo cha kupigia kura baada ya shughuli ya kupiga kura.

Mmoja wa maafisa wa GSU alitilia shaka mshukiwa baada ya kuona kitu kimefichwa kiunoni mwake.

Maafisa hao walimfunga pingu mshukiwa na kumwamuru alale chini, ambapo walimkuta akiwa na silaha hizo ghafi.

Alikabidhiwa kwa maafisa walio katika Kituo cha Polisi cha Homa Bay ambapo anazuiliwa kwa mahojiano zaidi.