Mgombea urais kwa tikiti ya chama cha Agano, David Mwaure amepiga kura yake na kuonesha furaha yake na kusema kwamaba amepiga kura yake.
Alisema kwamba wakati huu wa taifa kuchagua viongozi kwake ni kama wakati wa Mandera au Obama, wakati wa kusonga mbele baada ya mateso.
Alisema kwamba yeye kama mgombea mwingine yeyote anatarajia kushinda na kuingia na fagio kubwa ya kufagia uchafu wote na kuanza upya.
“Ninatarajia kushinda, ninatarajia Wakenya kunipigia kura na hiyo ndio ndoto yangu, nitaiongia na fagio langu kubwa na kuifanya Kenya kuwa nzuri tena kama inavyotakikana” Mwaure alisema baada ya kupiga kura yake.
Aidha alisema kwamba ikitokea amepoteza basi atakubali matokeo ya kumpa mkono yule ambaye atakuwa amechaguliwa kama rais.
Aliwataka Wakenya kujitokeza kupiga kura kwa kusema kwamba hata kama ni Mungu anatoa viongozi lakini anawatumia watu kufanya uchaguzi na maamuzi.
“Hata kama ni Mungu ambaye anatoa viongozi lakini huwacanatumia wanadamu kufanya maamuzi, unakuwa pale na uhatekeleza agizo takatifu na sababu mumekuwa mkiomba, Mungu atajibu maombi yenu leo,” Alisema Mtumishi wa Mungu, Mwaure.