"Pigeni kura kwa busara, uamuzi uko mikononi mwenu" Ruto awashauri wapiga kura

DP pia alionyesha imani kuwa Wakenya watafanya maamuzi sahihi.

Muhtasari

•Hili litakuwa jaribio lake la kwanza kuwania urais baada ya kuwa naibu wa Uhuru Kenyatta kwa miaka 10 iliyopita.

•DP pia alionyesha imani kwamba Wakenya watafanya maamuzi sahihi.

DP William Ruto akiwa katika kituo cha piga kura cha Sugoi
DP William Ruto akiwa katika kituo cha piga kura cha Sugoi
Image: screengrab

Naibu Rais William Ruto alfajiri ya Jumanne alitangulia kama mfano kuwa wa kwanza kupiga kura huku akiwarai wafuasi wake kutii ahadi ambayo wamekuwa wakitoa kwamba watarauka alfajiri kupigia kura muungano wa Kenya Kwanza.

Akizungumza huko Sugoi nyumbani kwao ambako alipiga kura yake alfajiri ya saa kumi na mbili, Ruto akitoa wito kwa Wakenya huku akiwaambia kwamba hii ndio nafasi yao muhali kufanya mageuzi katika uongozi ambayo wangependa kuyaona katika miaka mitano ijayo.

Ruto aliwataka Wakenya kupiga kura kwa amani.

“Kwa Wakenya, fanyeni zoezi hili na muende kupiga kura kwa amani, kwa makusudi na kwa uhakika ili tuchague wanaume na wanawake wanaoweza kuipeleka Kenya kwenye ngazi nyingine,” aliongeza.

 

Naibu rais ambaye yuko kwenye kinyang’anyiro hicho kujaribu bahati yake kuwa mrithi wa rais anayeondoka Kenyatta, pia alionyesha imani kuwa Wakenya watafanya maamuzi sahihi.

 

"Ni wakati ambapo wenye nguvu na wenye nguvu hugundua kuwa ni Wakenya wanaofanya chaguo. Kila Mkenya atachagua viongozi wake," alinukuliwa.

 

Hili litakuwa jaribio lake la kwanza kuwania kiti cha urais baada ya kuhudumu kama naibu wa Rais Uhuru Kenyatta kwa miaka 10 iliyopita.

 

Iwapo atachaguliwa kuwa rais katika kinyang'anyiro cha mwaka huu kinachotajwa kuwa na ushindani mkali kuwahi kushuhudiwa nchini tangu uhuru, akimenyana na aliyekuwa kiongozi wa upinzani Raila Odinga, itakuwa ni mara ya kwanza kwa mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 55.

Ruto anaelekea kwenye uchaguzi huu akiwa na Imani kubwa kuchaguliwa na katika kipindi cha kampeni zake amekuwa akinadi manifesto yake kama moja inayonuiwa kukomoa nchi kutoka kwa umaskini kwa kuimarisha uchumi.