MC Jessy Akubali Kushindwa Ubunge South Imenti

Binafsi nataka kumpongeza mshindani wangu anayestahili Dk Shadrack anapojitayarisha kuwa Mbunge mpya wa Imenti Kusini - MC Jessy.

Muhtasari

• Jessy alikuwa anawania kama mgombea huru baada ya kunyimwa tikiti ya chama cha UDA

Mchekeshaji na mwanasiasa Jasper Muthomi almaarufu MC Jessy
Mchekeshaji na mwanasiasa Jasper Muthomi almaarufu MC Jessy
Image: INSTAGRAM//MC JESSY

Mchekeshaji Jasper Muthomi almaarufu MC Jessy amebwagwa katika uchaguzi wa ubunge Imenti ya Kusini na mshindani wake mkuu Dkt. Shadrack katika kinyang’anyiro hicho.

Jessy amejiunga na wanasiasa wengine wengi ambao wakeridhia matokeo hayo na amekubali kushindwa huku akimpongeza Dkt. Shadrack kwa ushindi huo huku akimtakia kila la kheri katika kuwafanyia wana Imenti Kusini kazi.

“Kwa Wananchi wa Eneo Bunge la Imenti Kusini, Ninawashukuru kwa Dhati kwa muda ambao tumetangamana wakati wa kampeni zetu. Imekuwa safari nzuri. Safari ya matukio ya ajabu ya kisiasa. Safari ya mioyo yenye ujasiri. Tutaendelea kushiriki tunapotarajia Wakati Ujao. Mungu akipenda. Binafsi nataka kumpongeza mshindani wangu anayestahili Dk Shadrack anapojitayarisha kuwa Mbunge mpya wa Imenti Kusini. Kwa wafuasi wangu jipeni moyo ni Siasa tu, tuendelee kusonga Imenti Kusini kama Jumuiya moja Kubwa,” Jasper Muthomi aliandika kwenye Instagram yake.

Awali kulikuwa na utata baada ya mchekeshaji huyo kusemekana kwamba amejitoa kwenye kinyang’anyiro ambapo alikuwa na nia ya kuwania kwa tikiti ya chama cha UDA ila baada ya tikiti hiyo kupewa kwa mshindani mwingine kweney kura za mchujo kwa jina Mwiti Kathaara.

Naibu rais William Ruto alikuwa ametangaza kwenye Twitter yake akisema kwamba Jessy angepokea kazi katika kamati ya kampeni zake ila muda mchache baadae alijitokeza wazi na kupinga madai hayo huku akisema kwamba atakuwa debeni kama mgombea huru.